Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Jacob Bega amefanya ziara Kata ya Nyansurura na Rung’abure akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Ayub Mwita Makuruma pamoja na Afisa Mipango Mwandamizi Ndugu Martin Mlelema ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
Ziara ilianzia Kata ya Nyansurura, lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kusikiliza kero pamoja na mipango ambayo Kata imejiwekea kwa ajili ya kukamilisha shughuli za maendeleo, akiwakaribisha viongozi hao Diwani wa Kata hio Mheshimiwa Joeseph Seronga aliwathibitishia viongozi hao kuwa kazi imeanza Kata ya Nyansurura na kwamba yeye pamoja na wataalam walioko katika Kata hio wamejipanga kufanya kazi kwa kushirikiana.
Taarifa ya Kata hio ilisomwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Ndugu Damas Elias Nyantito ambayo ilionesha changamoto na mafanikio walioyapata kwenye shughuli za Maendeleo nakwamba wamepokea fedha Tsh 10,000,000/= kwa ajili ya kupaua Zahanati ya Nyansurura,Mabati 70, Mbao 360, Mifuko ya Saruji pia Tsh 2,525,000/= zimetengwa kwa ajili ya kujenga josho. Pamoja na mafanikio hayo alitaja changamoto ikiwa ni pamoja na upungufu wa madawati ,wanafunzi kukosa chakula shuleni.
Ziara ilihitimishwa Kata ya Rung’abure ambapo pia viongozi hao walipokelewa na viongozi wa Kata hio akiwemo Diwani wa Kata hio Mheshimiwa Samwel Nguti pamoja na wataalam ngazi ya Kata ambao walishukuru viongozi kufika katika Kata hio.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi aliwaambia lengo la ziara hio ni kuwashukuru kwa ajili ya ushindi kwa viongozi waliopatikana lakini pia kusikiliza kero kwenye Kata hio.
Kata ya Rung’abure ni moja ya Kata ambazo zimepokea vifaa toka Halmashauri ya Wilaya Serengeti ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wananchi, Diwani wa Kata hio amethibitisha kuwa wamepokea vifaa kwa ajili ya Shule ya Sekondari Gesarya Mabati 180,Mbao 300,Saruji Mifuko 50 pia, Ruwasa imelipa Tanesco Tsh 97,984,000/= kwa ajili ya kutengeneza miundo mbinu ya Umeme ili Wananchi waweze kupata Maji ya Uhakika.
Kata hiyo imejiwekea mkakati wa kujenga Shule ya Sekondari kila Kijiji na wameanza Shule ya Sekondari Gesarya, Kijiji cha Nyamerama pia tayari wameanza kupeleka viashiria kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari Nyamerama Mheshimiwa Samwel Nguti amesema lengo hilo la kuwa na Sekondari kila Kjiji ni maandalizi ya kuifanya Ikorongo Sekondari kuwa ya Kidato chaTano na cha Sita.
Afisa Mtendaji wa Kijiji Gesarya Bi Theresia Marwa amethibitisha kuwa Halmashauri ilitoa Tsh 5,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya Walimu wawili kwenye jengo moja Shule ya Sekondari Gesarya pamoja na mchango huo wa Halmashauri wananachi bado wanasuasua hivo waongeze bidii ili kukamilisha jengo hilo.
Imetolewa
Afisa Habari- Mahusiano
Emmanuel Isyaga Mwita
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti