Mkuu wa Wilaya ya Serengeti ,Mheshimiwa Nurdin Babu amekemea vitendo vya wanaume Wilayani humo kuwapiga na kuwanyanyasa Wanawake na Watoto wa Kike na kwamba wahakikishe watoto wote wanapata elimu sambamba na kuwalinda dhidi ya vitendo viovu.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Wilayani Serengeti ambayo yamefanyika Kata ya Mbalibali kiwilaya Mheshimiwa Babu amesema kuwa suala la ulinzi na usalama wa mtoto wa kike ni jukumu la kila mtu katika jamii lakini msingi wake unaanzia kwa wanawake na kwamba ili kuwa na Taifa lenye ustawi ulinzi wa mtoto ni jambo la muhimu.
Kuhusu suala la wanawake kupigwa Mheshimiwa Babu amekea jambo hilo na kwamba wanaume wenye tabia waache amesemakuwa wanawake na wanaume wanatakiwa kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata elimu sawa bila ubaguzi wa aina yoyote na kwamba serikali kwa kutambua umhimu wa elimu kwa watoto wote wa Tanzania imeamua kutoa elimu bila malipo hivyo ni jukumu la wanawake kuhakikisha kuwa watoto wote wanapelekwa shule ili wapate elimu kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa wanawake wana haki ya kusaidiwa na wajibu wa serikali kuhakikisha inawalinda na kuwakwamua kutoka majanga ya manyanyaso pia amehahidi kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Serengeti ambaye aliwakilishwa katika maazimisho na hayo na Ndugu Sunday Wambura Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Serengeti maazimisho ambayo yalihudhuliwa pia na Katibu Tawala(W) Ndugu Qamara Cosmas pamoja na watumishi toka idara mbali mbali Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
Imeandaliwa na:
Emmauel Isyaga Mwita
Afisa Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
09/03/2021.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti