MAAFISA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI WAFANYA KIKAO KAZI NA MKURUGENZI MTENDAJI(W) PAMOJA NA WATAALAM LENGO LIKIWA NI KUONGEZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO
Mkurugenzi Mtendaji(W)Eng Juma Hamsini leo 07/05/2021 amefungua Kikao Kazi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kuhudhuliwa na Watendaji wa Kata 30 pamoja na Vijiji 78 lengo hasa la Kikao hicho likiwa ni kuelimishana juu ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa Mapato kwenye maeneo yao ya kazi lakini pia kukumbushana majukumu yao mbali mbali.
Mara baada ya kufungua Kikao Mkurugenzi Mtendaji Eng Juma Hamsini aliwasihi Maafisa hao wa Serikali kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato bila kumuonea mfanyabiashara yoyote wafuate sheria na kanuni kwenye utendaji na mafanikio yataonekana.
Sambamba na hilo Bwana Sunday Wambura ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii alipata nafasi ya kuwakumbusha Maafisa Watendaji majukumu yao na kwamba wao ni wawakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji(W) hivyo wasiogope kufanya kazi ya kusimamia majukumu kwa mujibu wa sheria.
Bi Veronica Christopher ni Mwanasheria wa Halmashauri alitumia muda wake kuwakumbusha Maafisa Watendaji wa Vijiji majukumu yao hasa kusimamia vikao vya kisheria kwenye Vijiji vyao pamoja na Mikutano ya kisheria kwenye vijiji vyao kwa kila robo ambayo inajumuisha usomaji wa Mapato na Matumizi kwenye vijiji vyao.
Kupitia kikao hicho Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Bwana Dinary Gimery alipata wasaa wa kuwakumbusha Maafisa Watendaji hao juu ya uandaji taarifa ya Mapato na Matumizi kwenye vijiji vyao.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti