Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania (Mkurabita) chini ya Ofisi ya Rais wakishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti watoa mafunzo ya ujasiliamali kwa wananchi wa Kijiji cha Robanda kilichopo katika Kata ya Ikoma Wilayani Serengeti.
Mafunzo hayo yaliyojikita katika kujenga uwezo kwa wakulima na vyama vya wakulima yamefanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 1 mpaka 3 mwezi Februari 2018 katika ofisi za Kata yameonekena kutoa mwanga wa wananchi huku wakitakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji na kunufaika na mikopo kutoka taasisi za fedha.
Bwana Antony Temu ambaye ni meneja urasimishaji rasilimali ardhi vijijini kutoka MKURABITA anasema kuwa “Mafunzo haya yatawafungua wananchi juu ya fursa zilizopo hapa robanda na kuzitumia kujiongezea kipato” anaendela kwa kusema “Tuna lengo la kubadilisha mtazamo wa wakulima ili kuwa na kilimo endelevu chenye tija ndio maana tumezialika taasisi za fedha ili wapate elimu ya mikopo na kuona namna wanavyoweza kunufaika na mikopo hiyo”
Taasisi za fedha (benki) za NMB na CRDB zote kutoka Wilayani Serengeti zilipata nafasi ya kutoa mada kwa wananchi hao huku wakibanisha fursa walizonazo wananchi katika kuhifadhi fedha zao na kupata mikopo.
Bwana Edwin Costantine afisa mikopo kutoka benki ya CRDB anabainisha kuwa hati miliki ya kimila pekee haimwezeshi mtu kupata mikopo na kuwataka wananchi kutumia elimu waliyopata juu ya kuanzisha biashara, kutunza nyaraka na kuandaa maandiko mradi kuomba mikopo ambapo hati miliki hutumika kama dhamana ya mikopo hiyo. Huku Bwana Elvis Kokia afisa mikopo kutoka Benki ya NMB akisema kuwa lengo la taasisi za fedha katika kutoa mikopo ni kumsaidia mteja kutimiza malengo yake na sio kumpora hati yake baada ya kushindwa kurudisha fedha huku akiwasihi waombaji wa mikopo kuwa na malengo pindi wanapoomba mikopo kutoka taasisi za fedha.
Mzee Samson Wahika mkazi wa Kijiji cha Robanda hakusita kutoa maoni yake juu ya mafunzo hayo kwa kusema “Mafuzo haya yatanisaidia kwenda kuboresha shamba langu na kuliongezea thamani kwa kulima mazao ya biashara” aliendelea kwa kuomba mafunzo hayo yafike na sehemu nyingine Wilayani Serengeti na Taifa kwa ujumla ili wananchi wanufaike na rasilimali zao.
Katika mafunzo hayo ya siku tatu mada mbalimbali zilitolewa kutoka maafisa ardhi, kilimo, mifugo, maendeleo ya jamii pamoja na ushirika wote kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambapo wananchi walielimishwa kuhusu umuhimu wa utunzaji wa nyaraka, elimu ya kilimo cha biashara, kuongeza thamani ya ardhi, kuandaa maandiko ya miradi pamoja na kudumisha vyama vya ushirika.
Aidha wananchi hao wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo kutoka Halmashauri kwa kuunda vikundi vya wanawake na vijana na kuwa na shughuli ya kiuchumi ili kuweza kupata mikopo kutoka Halmashauri.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Robanda Mheshimiwa Mrobanda Japan akifungua mafunzo ua ujengaji uwezo kwa wakulima wa Kijiji cha Robanda.
Bwana Antony Temu Menejan urasimishaji rasilimali ardhi vijijini kutoka MKURABITA akitoa mada kwa wananchi wa robanda.
Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Bi. Eliza Simon (aliyesimama) akitoa mafunzo kwa wananchi wa Kijiji cha Robanda.
Bwana Edwin Constantine afisa mikopo kutoka Benki ya CRDB Serengeti akitoa mada kwa wananchi wa Kijiji cha Robanda.
Bwana Elvis Kokia kutoka Benki ya NMb akitoa mada kwa wananchi wa Kijiji cha Robanda.
Mzee Samson Wahika mkazi wa Kijiji cha Robanda akisoma hati miliki ya kimila ya ardhi yake aliyopata baada ya urasimishaji wa ardhi yake.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti