Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambaye pia ni diwani wa kata ya Busawe Mhe. Ayoub Mwita Makuruma amewataka wananchi ya wa kata ya Nagusi kushirikiana na serikali ili kufanikisha ujenzi wa miradi mbalimbali katika maeneo yao.
Makuruma ameyasema hayo alipotembela ujenzi wa shule ya Sekondari Chifu Salota inayojengwa katika kata ya Nagusi na kufanya mkutano wa hadhara katika kata hiyo.
Aidha Mhe. Makuruma amewataka wananchi kuongeza nguvu katika uchangiaji wa viashiria ili ujenzi wa shule hiyo uweze kukamilika kwa wakati.
"nguvu ya wananchi ni ya muhimu Sana katika utekelezaji wa miradi, sehemu yenye nguvu ya wananchi haiwezi kukwama" alisema Makuruma
Vilevile Mhe.Makuruma amekemea vikali tabia ya udokozi wa vifaa wakati wa ujenzi wa Sekondari hiyo kwani kufanya hivyo ni kuhujumu jitihada za serikali katika kuleta maendeleo na kuwataka kushiriki katika ulinzi wa vifaa hivyo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Nagusi ameishukuru serikali kwa kuipa kipaumbele kata ya Nagusi kwani shule hiyo ikikamilika itaondoa adha kubwa ya watoto wao wanaotembea umbali mrefu kutafuta huduma ya elimu kata ya jirani.
Nao wananchi wa kata wamesema shule ya Sekondari kilikuwa kilio chao cha muda mrefu na kuaidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika ujenzi wa shule hiyo kwani kukamilika kwake kunamanufaa makubwa sana kwao.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti