Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambaye pia ni Diwani wa kata ya Busawe Mhe. Ayoub Mwita Makuruma amewataka viongozi wa Kata ya Nyamatare pamoja na Mganga mkuu wa wilaya kuhakikisha wanatumia busara ili wananchi waliovamia eneo la zahanati ya Kemgesi waondoke katika eneo hilo.
Wakati alipotembelea Zahanati hiyo Mhe. Makuruma amesema kitendo cha kuvamia eneo la zahanati kutaifanya zahanati hiyo kukosa eneo la kujenga majengo mengine ya kutolea huduma na hivyo kuifanya zahanati ishindwe kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
eneo la zahanati ya Kemgesi lililovamiwa na wanakijiji
Aidha, Mhe. Makuruma ametembelea ujenzi wa zahanati mpya ya Nyirongo iliopo kata ya Nyamatare inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo amepongeza juhudi za wakazi hao katika kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali
jengo la zahanati ya Nyirongo
Vilevile Mhe.Makuruma ametoa pongezi kwa mdau wa maendeleo Ndg. Rhimo Nyansaho ambaye ameshirikiana na wananchi katika kuezeka zahanati hiyo.
Mhe. Makaruma ameitimisha ziara yake katika kata ya Nyamatare kwa kuhudhuria mkutano wa hadhara katika kata hiyo ambapo amekaguaa majengo ya shule ya msingi Nyamatare.
na amewatakaa wananchi wa kata hiyo kuhudhuria mikutano mbalimbali inayoandaliwa na viongozi wao kwani kupitia mikutano hiyo ndipo sehemu sahihi ya kueleza changamoto zao.
Katika ziara hiyo Mhe. Makuruma ameambatana na baadhi ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na baadhi ya madiwani wa kata mbalimbali.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti