Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mh. Marwa Ryoba amewataka wananchi na wadau wote wa maendeleo Wilayani Kuhakikisha kuwa wanajenga Maboma ili Serikali Kuu nayo iweze kuchangia katika miradi mbali mbali.
Mh. Ryoba ameyasema hayo leo Katika Kijiji cha Kitunguruma kilichopo Kata ya Mbalibali wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ilipokuwa ikitembelea miradi mbalimbali ambayo miradi mingi fedha zake zinatokana na mpango wa lipa Kulingana na matokeo (P4R), Halmashauri pamoja na nguvu za wananchi
Bweni la wavulana katika shule ya sekondori Ngoreme likiwa bado halijakamilika
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango hufanya ziara zake za kutembelea miradi ya maendeleo kwa mujibu wa kanuni za kamati za kudumu za Halmashauri na lengo kuu pamoja na mambo mengine ni kuona na kutathimini thamani ya fedha pale ilipotekelezwa, kushauri na kuhamasisha jamii katika kuchangia miradi ya maendeleo.
Moja ya darasa katika Shule ya sekondari Nyansurura
Akizunguza mara baada ya kamati hiyo kukagua ukamilishaji wa madarasa matano katika Shule ya Sekondari Kitunguruma Mh. Ryoba amewataka wananchi na wadau wote kuhakikisha kuwa wanajitahidi kujenga majengo mengi wawezavyo ili Serikali Kuu nayo iweze kuchangia fedha kwa wingi.
Akitolea mfano Shule ya Kitunguruma ndio shule iliyopewa fedha nyingi kati ya Milioni mia tatu zilizopokelewa katika wilaya nzima kwani shule hiyo ilipewa Milioni Hamsini na hii ni kutokana na kuwa na maboma manne.
Baadhi ya madarasa katika shule ya sekondari Kitunguruma
Hivyo aliwasisitiza wananchi na wadau wote wa maendeleo kuhakikisha wanajenga maboma ya kutosha na amesema kuwa serikali imetenga na inategemea kuletea fedha nyingine kabla ya kuvunja kwa bunge tukufu.
Shule mpya inayoendelea kujengwa katika kijiji cha Musati Kata Kibanchebanche
Kamati Hii iliweza kutembelea miradi mbalimbali ambayo ni
Nyumba ya walimu "Six in one" katika Shule ya sekondari Natta
Wakati huo huo Mh. Ryoba amewaahidi watumishi wa Kata ya Busawe, Kenyamonta na Majimoto kwanunulia Jezi na Mpira wa miguu mmoja moja kwa kila kata hizo aidha amesema kuwa anafikiria kuanzisha ligi ya mpirta kbla ya mwezi Disemba mwaka huu huku akifikiria kuwa mshindi wa kwanza atapatiwa zawadi ya fedha Taslimu Milioni Moja na Mshindi wa pili fedha Taslimu laki sita na uku akisema mshindi watatu watapanga
Aliyasema hayo wakati akiwasalimia watumishi wa kata hizo waliokuwa wakifanya mazoezi katika uwanja wa michezo uliopo katika shule ya sekondari ya Ngoreme iliyopo katika Kata ya Kenyamonta.
Mh. Mbunge (Mwenye suti ya Bluu) pamoja na baadhi ya wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji watumishi kata ya Busawe, Kenyemonta na Majimoto
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti