Shule ya Sekondari Busawe iliyopo wilayani Serengeti Kata ya Busawe Mkoani wa Mara,imefanya mahafali yake ya 12 ya kidato cha nne katika shule hiyo,ambapo jumla ya wahitimu 106 walihitimu
Akiwa ni Mgeni katika mahafali hayo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti na diwani wa kata ya busawe Mhe.Ayub Mwita Makuruma(Prince Makuruma Omwana wa Baghaka omwana wa kyaro) amewapongeza wahitimu wote kwa kuweza kusoma kwa bidii na kuvumilia mapito yote na hatimaye kuweza kuhitimi masomo yako
‘’hongereni sana kwa uhitimu masomo yenu maana kati ya wanafunzi 154 nyie mmefanikiwa kuhitimu,hivyo mkaitumie elimu mliyipata kwa manufaa ya taifa alisema ‘’Makuruma
Aidha,Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa ebola ambao upo katika nchi jirani ya Uganda.
Mhe.Makuruma ameahidi kuwaendelea kuishika mkono shule hiyo sambamba na kuwa nao bega kwa bega katika Shughuli mbalimbali za kitaalumu na michezo.
Mahafali hayo yalipambwa burudani za nyimbo,maigizo,Maonyesho Mbalimbali na mashairi kutoka kwa wahitimu. Mahafali hayo yalihudhuriwa na walimu,wazazi,Ndugu,jamaa na marafiki
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti