Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambaye pia ni diwani wa kata ya Busawe, Mhe. Ayoub Mwita Makuruma katika kuunga mkono juhudi za serikali kuleta maendeleo ndani ya kata ya Morotonga, amechangia kiasi cha Shilingi Milioni moja ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Morotonga.
Mhe. Makuruma katika ziara yake ndani ya kata hiyo ameshiriki katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Kata hiyo ambapo amekabidhi kompyuta na printa zilozotolewa na mdau wa maendeleo.
Katika mkutano huo Mhe. Makuruma amewaasa viongozi wa chama Cha mapinduzi katika kata hiyo kidumisha ushirikiano sambamba na kuungu mkono jitihada za diwani wao katika kuwaletea maendeleo.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Mhe. Magasi Mseti amesema ataendelea kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo katika kuhakikisha analeta maendeleo ndani ya kata ya Morotonga.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti