Makundusi ni mojawapo ya vijiji vilivyokatika mkakati wa uhifadhi wa mazingira na wanyamapori wilayani Serengeti, katika kuhakikisha hilo linafanikiwa,uongozi wa kijiji hicho kupitia kwa mwenyekiti wake Ndg. Joseph Mseti kwa zaidi ya miaka saba sasa wamekuwa na desturi ya kutumia michezo mbalimbali maarufu Kama MAKUNDUSI CUP ili kuhamashisha uhifadhi wa mazingira na wanyamapori katika hifadhi zinazo zunguka Kijiji hicho.
Katika kilele cha fainali za mashindano ya "Makundusi cup" Ndg. Mseti amesema uongozi wa kijiji hicho utaendelea kushirikiana na wadau wa uhifadhi ili kuhakikisha mashindano hayo yanatimiza lengo kuu la uhifadhi katika Kijiji hicho sambamba na kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa endelevu kwani yamezaa matunda makubwa katika upande wa uhifadhi pamoja na kuimarisha afya za wakazi wa Kijiji hicho tangu yalipoanzishwa.
Naye Afisa mahusiano kutoka TAWA amewapongeza washindi katika mashindano hayo na kuaidi kuendelea kutoa ushirikiano katika mashindano hayo kwani wananchi wa Makundusi wamekuwa wadau namba moja wa uhifadhi na kuwataka kutumia Elimu waliyoipata wakatika wa mashindano hayo kuhifadhi mazingira na wanyamapori katika maeneo yao.
Kijiji Cha Makundusi kamamoja ya vijiji vilivyokatika mpango mkakati wa uhifadhi wa wanyamapori, kimepakana na hifadhi za Ikorongo na Grumet kila mwaka huandaa tamasha la michezo ili kuhamadisha uhifadhi ambapo husaidia kupunguza uwindaji haramu pamoja na kutoa elimu juu ya uhifadhi wa mazingira na namna ya kujikinga na wanyama waharibifu kama tembo.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti