Wanafunzi wa shule ya Sekondari Robanda iliyopo kata ya Ikoma Wilayani Serengeti wataanza kusoma kidigitali, baada ya kupokea ufadhili wa vifaa vya Tehama kompyuta 20 kutoka kwa mdau wa maendeleo Ndg. Rhimo Nyansaho.
Akitoa msaada huo katika mahafari ya nne ya shule hiyo alipokuwa mgeni rasmi Ndg. Nyansaho amesema kutokana na dunia ya sasa ya kidigitali ni vyema pia kuwaandaa wanafunzi kusoma kidigitali ili waweze kuendena na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Aidha Ndg. Nyansaho katika kuhakikisha wanafunzi wa shule hiyo wanapata elimu bora wawapo shuleni hapo ametoa vitanda 48 pamoja na magodoro 96 ili wanafunzi waweze kulala shuleni hapo, vilevile akihamasisha uhifadhi amewataka wahitimu wa shule hiyo kutumia elimu waliyoipata kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na wanyamapori.
kwa upande wake Katibu tawala wa Wilaya ya Serengeti Bi. Angella Marko amewaasa wahitimu kuyaweka katika vitendo yale yote waliyofundishwa na kuwataka wazazi kuwafundisha wahitimu hao kazi za nyumbani na shughuli za kujenga taifa na ikiwa ni pamoja na kidumisha uhifadhi na kuwataka kuunga mkono juhudi za kupinga uwindaji haramu.
Nao wahitimu wa shule ya Sekondari Robanda wameushukuru uongozi wa shule kwa kipindi chote walipokuwa shuleni hapo na kutoa shukrani zao kwa mgeni rasmi kwa namna ambavyo anaendelea kuchangia maendeleo katika sekta ya elimu.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti