Na Simeon Nashon Waryuba.
Ni mdudu ambaye kwa kiingereza hujulikana kama Fall Armyworm au kwa jina la kitaalamu “Spodoptera frugipedra” asili yake ni Bara la America. Mdudu huyu alionekana kwa mara ya kwanza katika nchi za Africa Magharibi (Nigeria) mwishoni mwa mwaka 2016.
Hadi mwezi February 2017, kiwavijeshi huyu alikuwa ameshavamia nchi za Afrika Kusini, Kati na Mashariki zikiwemo Zimbabwe, Msumbiji, Zambia, Congo na Rwanda. Hapa nchini kiwavijeshi vamizi aliripotiwa kwa mara ya kwanza katika wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa mwezi Machi 2017.
Hadi mwezi Disemba 2017 kiwavijeshi huyu alisharipotiwa kwenye mikoa zaidi ya 15 Maarufu kwa kilimo cha mahindi ikiwemo Mbeya, Shinyanga,Ruvuma, Iringa, Geita, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro,Tanga, Kigoma, Kagera, Mwanza, Pwani na Lindi.
Mzunguko wa Maisha ya Kiwavijeshi vamizi {Fall Armyworm}
Ukuaji wa mdudu huyu hupitia katika hatua nne za ukuaji ambazo ni; yai – kiwavi – buu – mdudu kamili (nondo). Hatua ya kiwavi ndiyo inayoshambulia na kuathiri mazao.
Mazao yanayoshambuliwa na Kiwavijeshi vamizi (Fall Armyworm)
Kiwavijeshi ( Spodopter frugipedra) hushambulia aina nyingi za Mazao mfano nafaka (Mahindi, Mtama,Mpunga) Mikunde, mbogamboga, (nyanya, mchicha, matikiti, pilipili) ,mbegu za mafuta (karanga, alizeti,pamba) ,miwa, matunda, (migomba, miembe, michungwa) pamoja na malisho ya mifugo mf. Mabingobingo.
Kiwavijeshi vamizi hushambuliwa mazao katika hatua zote za ukuaji kwa mfano mahindi hushambuliwa yakiwa bado machanga hadi wakati yameshakomaa hivyo kufanya udhibiti kuwa ngumu na wa gharama kubwa.
Dalili za uharibifu wa Kiwavijeshi Vamizi kwenye zao la Mahindi.
Wadudu wanavyoonekana katika sehemu ya mmea unapoota.
Mdudu akishambulia kwenye gunzi ka Mhindi
Jinsi ya Kudhibiti Kiwavijeshi Vamizi (Fall Armyworm)
Udhibiti wa kibaiolojia
Mdudu huyu anaweza kudhibitiwa kwa njia ya matumizi ya wadudu au viumbe marafiki kama vile Manyingu mf. Telenomus spp, Earwings, na Kuvu mf. Beauvera bassiana ,Bacillus thrugiensis n.k hata vivyo njia hii inahitaji maandalizi maalumu nap engine inaweza kuchukua muda mrefu kwa sababu ni lazima wadudu marafiki wawe wa kutosha.
Udhibiti Sango
Udhibiti wa kutumia Viuatilifu
Matumizi ya kiuatilifu iwe ni hatua ya mwisho baada ya mbinu nyingine kushindwa
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti