Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Ayub Mwita Makuruma, jana Aprili 15, 2025 umefanya ziara katika eneo linapojengwa jengwa jengo la Utawala la halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kushiriki katika hatua za awali za ujenzi wa jengo hilo ikiwa ni pamoja na umwagaji wa zege.
Wakati wa ziara, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni mwenyeti wa Halmashauri Mhe. Ayub Mwita Makuruma ameshauri kuwepo kwa usimamizi mzuri wa mradi huo ili uweze kumalizika kwa wakati.
Ujenzi wa jengo la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, unaotekelezwa chini ya Mkandarasi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika eneo la Bomautagharimu shilingi bilioni 4.5 ambapo katika awamu ya kwanza halmashauri imepokea kiasi cha shilingi Milioni 740.
Aidha, mradi huo unahusisha ujenzi wa jengo moja la ghorofa moja ambalo litabeba ofısi zote za halmashauri sambamba na kumbi mbili za kisasa zitakazotumika katika vikao na mikutano mbalimbali ya Wilaya.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti