Tarehe 25 Aprili ya kila mwaka ni siku ya Malaria duniani, ni wakati ambapo Shirika la Afya duniani (WHO) hutoa uelewa kwa ujumla kuhusu juhudi za pamoja na kuiepusha dunia na malaria.
Nchini Tanzania, Takwimu zinaonesha kuwa maambukizi ya ugonjwa wa Malaria nchini yameendelea kupungua katika kipindi cha miaka saba kwa asilimia 45 kutoka asilimia 14.8 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 8.1 mwaka 2022 huku idadi ya vifo vitokanavyo na Malaria ikipungua kwa asilimia 39 kutoka vifo 2460 mwaka 2020 hadi kufikia vifo 1503 mwaka 2024.
Wilayani Serengeti, katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza mikakati na afua mbalimbali za kupambana na ugonjwa huo, Idara ya Afya Wilayani Serengeti, imetumia siku hii kuendesha zoezi la upimaji wa malaria kwa wananchi na Wanafunzi waliojitokeza katika shule ya Msingi Kambarage A sambamba na kutoa elimu juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa malaria pamoja na namna ya kutambua dalili za ugonjwa huo.
Katika siku hiyo iliyobeba kauli mbiu isemayo Malaria inatokomezwa na sisi: wekeza, chukua hatua- Ziro Malaria inaanza na Mimi" wananchi wameaswa kuzingatia matumizi ya dawa za Maleria pamoja na kuzingatia matumizi ya chandarua.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti