Baraza la madiwani Wilayani Serengeti kwa kauli moja limepitisha mapendekezo ya bajeti ya Wakala wa barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.4 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Akiwasilisha mpango huo wa bajeti mbele ya Baraza la madiwani, Meneja wa TARURA Wilaya ya Serengeti Mhandisi Frank J. Moshi amesema "bajeti hii inahusisha matengenezo ya barabara kutoka Mfuko wa barabara, fedha za maendeleo va shilingi milioni 894.9 kwa ajili ya barabara, shilingi Milioni 500 nyongeza ya bajeti kwa jimbo na shilingi milioni 1000 Tltozo ya mafuta ya petrol na dizeli kutoka Serikali Kuu".
Aidha, makadirio haya ya Bajeti yanalenga kukamilisha jumla ya km 115.66 matengenezo ya kawaida na Ujenzi wa Makalavati 16 kwa fedha za Mfuko wa Barabara. Km 26.87 za matengenezo ya muda maalum, Ujenzi wa daraja moja 1, Ujenzi wa Makalavati 21 na Ufungaji wa taa 20 barabarani kwa fedha za Tozo ya mafuta ya petrol na dizeli. Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami nyepesi Km 0.270 pamoja na ufungaji wa taa 20 za barabarani kwa fedha za nyongeza ya bajeti ya mfuko wa jimbo.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti