Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Jeremiah Mrimi Amsabi amekabidhi gari la wagonjwa katika Kituo cha Afya Iramba kilichopo katika kata ya Kenyamonta Wilayani Serengeti ambapo gari hiyo itasaidia kutoa huduma kwa wakazi ya Kenyamonta na maeneo ya jirani.
Katika hafla ya kukabidhi gari hilo iliyofanyika katika kituo cha Afya Iramba, Mhe. Amsabi amewaomba wananchi hao kutunza gari hiyo na kuitumia katika shughuli za kituo cha Afya hicho na si vinginevyo.
Kwa upande wake Mganga mkuuywa Wilaya ya Serengeti kwa niamba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Dkt. Lusubilo Adam ameaidi kuusimamia uongozi wa kituo cha Afya Iramba kuhakikisha gari hiyo inatumika kwa matumizi sahihi na kuishukuru Serikali kwa namna inavyozidi kuiboresha sekta ya Afya Wilayani Serengeti.
Nao wananchi wa Kata ya Kenyamonta wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboreshea huduma bora za matibabu na kunusuru maisha yao kwani gari hiyo itawaondolea changamoto kubwa iliyowakabili wanawake wajawazito na wagonjwa wengine ya kukosa usafiri wa haraka ili kuokoa maisha yao pindi wanapoumwa.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti