Kamati ya fedha, uongozi, na mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub Mwita Makuruma imetembelewa na kukaguliwa Vyumba viwili vya madarasa shule ya Sekondari Nyichoka
Shule ya Nyichoka Sekondari ilipokea Fedha tsh. Milioni Arobaini (40,000,000) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ,mpaka sasa Mradi umekamilika na uko kwenye matumizi kwa wanafunzi walio andikishwa mwaka 2023 Ujenzi umefanyika kwa kuzingatia miongozo ya serikali na kwa ushrikiano mkubwa wa kamati zote za ujenzi.
Uongozi wa Sekondari Nyichoka unapenda kutoa Shukrani za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona haja ya kuendelea kuleta miradi kwa wanajamii wa Nyichoka ili jamii iendelee kunufaika katika sekta Mbalimbali ikiwemo elimu.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti