Hospitali ya wilaya ya Serengeti iliyoko katika kitongoji cha Kibeyo katika Kata ya Kisangura inatarajiwa kuanza kutoa Huduma zake tarehe 01/03/2019
Jengo la huduma ya mama na mtoto
Hayo yalibainishwa na Katibu wa Afya Wilaya Bw. Peter Shillingi katika ziara ya kawaida ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Mhandisi Juma Hamsini alipokuwa akitembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo leo tarehe 20/02/2019.
“Tayari menejimenti imeshahamia hapa hospitali na tunategemea jumatatu ya tarehe 28/02/2019 watumishi waliobaki kule Hospitali Teule wahamie hapa na tunatarajia pia tarehe 01/03/2019 tuanze kutoa huduma kwa kuanza na huduma za mama na mtoto (RCH), meno, Dawa (Phamacy), Maabara pamoja na Hudumu za CTC (Huduma za Kliniki kwa Waathirika wa Virusi vya UKIMWI)” Alisema Bw. Shillingi
Naye Mhandisi Juma alisistiza kuwa wahakikishie wanakamilisha taratibu zote za kuhamia hospitalini hapo na kuanza kutoa huduma hizo mara moja.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti