Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Vincent Mashinji amemtaka mtendaji wa kijiji cha Nyanungu kukamilisha ukusanya wa ahadi zilizotolewa kwenye harambee ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyanungu haraka iwezekavyo ili ujenzi wa sekondari hiyo usikwame
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kijiji hicho Dkt. Mashinji amesema kuwa ujenzi wa shule ya sekondari Nyanungu unatakiwa kwenda kwa kasi ili mwakani shule hiyo iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza hivyo akamtaka tendaji huyo kufuatilia ahadi zote zilizotolewa na wadau siku ya harambee ya ujenzi wa sekondari hiyo.
"Kama shida ni kuwaandikia barua kwanini usiandike? haiwezekani tangu harambee imefanyika miezi karibia mitano imepita bado hujakamilisha ukusanyaji wa ahadi zote zilizotolewa, kufikia alhamisi nataka uwe umekamilisha kukusanya ahadi hizo na uniandikie taarifa" alisema Dkt. Mashinji
Ujenzi wa shule ya sekondari Nyanungu unatarajiwa kukamilika ifikapo mwenzi Septemba ambapo shule hiyo inajengwa kwa nguvu za wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kushirikiana na serikali.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti