Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Vincent Mashinji ameyafunga machimbo ya matare yaliyopo kitongoji cha kanisani kufuatia kifo cha Mchimbaji wa kokoto Sendi Chacha Nyantori (16) mara baada ya kufukiwa na kifusi wakati akichimba mawe ambapo wengine wawili wamejeruhiwa .
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Vincent Mashinji Akizungumza na wachimbaji wa kokoto katika eneo la Matare
DC mashinji amewataka wachimbaji hao wa kokoko katika machimbo hayo kutoendelea na shughuli za uchimbaji mpaka pale wataalamu kutoka ngazi ya wilaya na Mkoa watakapofanya utafiti na kuhakikisha hakutakuwa na madhara katika uchimbaji katika eneo hilo
‘’tunataka mtu anapokwenda kutafuta ridhiki awe na uhakika wa kurudi nyumbani,kazi hii ni Halali kama zilivyo kazi nyingine,ila kwa sasa tunayafunga mchimbo haya mpaka pale mtakapotaarifa tena baadaya ya wataalmu kujiridhisha na hali ya usalama wa uchimbaji katika eneo hili’’amesema Mashinji.
Ameongeza pia wote ambao waliponda kokoto zao kwa ajili ya kuuza wanaweza kuziuza .
Kwa upande wa wachimbaji katika eneo hilo wameridhia na takwa na DC mashinji na kupasauti zao kwa serikali kuomba kuwekewa mazingira rafiki katika eneo hilo ili waweze kujikidhi kiuchumi.
Katika mashimo haya ya kokoto Mwaka 2013 watu wengine wawili walikufa kwa kuangukiwa na udongo wakati wanachimba kokoto.
Waliojeruhiwa katika tukio hilo ni Nyamhanga Mwikwabe Kisara(55)ambaye amelazwa hospitali ya Nyerere na Esther Daniel (23)ambaye ni mke wa kijana wake ambaye amepata majeraha madogo madogo,wote wakazi wa kitongoji cha Kanisani Matare.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti