Chama cha walimu Tanzania Wilayani Serengeti kimetoa Baiskeli 5 zenye thamani ya Tsh 975,000/=kwa baadhi ya walimu wenye ulemavu kutoka shule za msingi ili ziwasaidie katika kutelekeza majukumu yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuwai kufika kazini.
Akikabidhi baiskeli hizo kwa walimu hao mgeni rasmi katika hafla hiyo mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Vincent Mashinji amekipongeza chama cha walimu Serengeti kwa kulitambau kundi hilo na kulishika mkono na kuwahimiza nguvu kubwa kuwekeza kwenye maendeleo ya chama chao .
Mwenyekiti wa CWT wilaya ya Serengeti Mwl.Mayala Lusawi amepongeza walimu wenye hali za ulemavu kwa kuwa mstari wa mbele katika kutelekeza majukumu yao na kuwa mchango mkubwa katika Jamii,akaongeza pia dhumuni la kupewa baiskeli hizo ni kuwarahisishia majukumu yao ya kila siku na kuwataka kuzitumia basikeli hizo kwa malengo yaliyokusudiwa
‘’Imetupendeza wenzetu hawa wenye mahitaji maalumu tuwawezeshe vifaa hivi vya usafiri angalau wawe wanaweza kufika kwa urahisi na kwa uharaka Zaidi katika vituo vyao vya kazi, hili wazo ni endelevu na tumetoa vifaa hivi kulingana na mahitaji yao’’Alisema Mayala
Nae,Katibu wa CWT Serengeti Ndg. Cloford Mkwama amesema ‘’Baiskeli hizi zitawasaidia Ndugu zetu hawa waweze kufika kazini kwa wakati,ili waweze kutimiza wajibu wao’’
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Mara ndugu Abdallah Malima amesema huu ni mwanzo na kama chama kitaendelea kutoa vitendea kazi na sapoti kwa walimu ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo
Kwa upande wa Katibu wa CWT Mkoa wa Mara Sussane Shesha ameupongeza uongozi wa CWT Wilaya ya Serengeti kwa utoaji wa baiskeli na kuzitaka wilaya nyingine kuiga mfano huu,aidha ameikumbusha serikali kuendelea kuboresha mazingira kwa kwa ajili ya walimu wenye ulemavu
Kwa niaba ya walimu wenye ulemavu Mwl.Okayo Misolo amesema wanakishukuru chama chao kwa kutambua uwepo wao na wameahidi kufanya kwa kazi kwa biddi kwa kushirikiana na viongozi .
Sambamba na hafla hiyo ya ugawaji wa baiskeli CWT Serengeti iliendesha pia zoezi la uchaguzi la kuziba nafasi ya muakilishi wa vijana wa CWT serengeti nafasi hiyo ilikuwa inagombewa na watu 6.ambapo ndugu Muhochi machugu alishinda nafasi hiyo.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti