Benki ya Azania Tawi la Serengeti katika kuhakikisha inamuinua mwanamke kiuchumi imezindua rasmi akaunti ya mwanamke Hodari ambayo itamuwezesha mwanamke kupata mkopo wenye riba nafuu kwa ajiri ya kuwainua wanawake wajasiriamali wilayani Serengeti.
Akizungumza katika uzinduzi wa akaunti hiyo meneja wa Azania bank Serengeti Bi.Elizabeth Koboko amesema ‘’ baada ya kugundua kuwa wanawake wengi nchini wanapata changamoto ya kupata mikopo,benki ya Azania imeamua kuja na akaunti ambayo itamuwezesha mwanamke kupata mkopo kuanzia laki 2 Hadi milioni 500 wenye riba ya asilimia moja tu,kwa mwezi ili kuwainua wanawake wote nchini kiuchumi.
Koboko ameongeza kuwa adhima ya benki ya Azania ni kuwainua wananchi wote kiuchumi hivyo benk hiyo imeamua kuanza kutoa huduma hiyo sambamba na kutoa elimu ya kifedha kwa wanawake hao.
"Benki ya Azania baada ya kugundua kuwa wanawake wengi wanachangamoto ya kupata mikopo na kuogopa kuweka fedha zao benki kwa kuogopa Makato makubwa, benki ya Azania imekuja na akaunti ambayo inafunguliwa bure hata anapotoa fedha yake katika akaunti hii ni bure ndio maana Benki ya azania imemrahisishia mwanamke kupitia akaunti hii ili apate sifa za kukopesheka" alisema Koboko
Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya Serengeti Angella Marko amewataka wanawake wote kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na benki ya azania kwa kubuni miradi mbalimbali itakayowawezesha kukopesheka na kurejesha fedha hizo kwa wakati.
Aidha Bi.Angella ameipongeza Benki hiyo kwa namna ambavyo inajitoa katika jamii kwa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia S.Hassan katika kuwakwamua wananchi wote kiuchumi.
"Tusaidianeni wanawake katika vikundi ili tuweze kunufaika na mkopo huo ili tuweze kuwa na nguvu kiuchumi kwani mwanamke akiwa na uchumi katika jamii hata manyanyaso hupungua" alisema Angella
Nao baadhi ya wanawake wa wilaya ya Serengeti wameishukuru benki ya azania kwa kuja na huduma hii kwani itawafanya wao kuinuka kiuchumi na kuwashauri wanawake wezako kuchangamkia fursa hiyo.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti