Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambae pia ni Diwani wa Kata ya Busawe Mhe.Ayub Makuruma amewasisitiza madiwani wilayani Serengeti kuendelea kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato,sambamba na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Shughuli za maendeleo.
Makuruma ameyasema hayo wakati wa mkutano wa baraza la madiwani lililofanyika mei 25,2023 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti.
Aidha kupitia baraza hilo waheshimiwa madiwani kutoka kata 30 walitoa mrejesho wa shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo wakigusia mafanikio na changamoto zilizojitokeza.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mkutano wa baraza la madiwani.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti