Wednesday 22nd, January 2025
@VIWANJA VYA RIGHT TO PLAY
MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA TANZANIA
Kila ifikiapo Julai 25 ya kila Mwaka,Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza Maisha yao wakiutetea,Kuupigania na Kulinda Uhuru wa Tanzania. Siku hii pia huambatana na Shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalumu za kuwaombea Mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea Amani ya Nchi kutoka kwa Viongozi wa Dini.
Mashujaa hao walipambana kwa Hali na mali kwa ajili ya kuitetea Nchi ya Tanzania wakiwa katika Maeneo Mbalimbali.Walijizatiti na kujitoa kwa uzalendo mkubwa kwa kuweka rehani Maisha yao kwa ajili ya Tanzania.Uongozi na menejimenti ya Wilaya ya Serengeti tunaungana na Watanzania wote kuwakumbuka na kuwaombea kheri kutokana na kujali na kudumisha Misingi ya Amani.
Misingi mizuri na imara iliyojengwa wasisi wa Taifa letu baba wa Taifa ,Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere Na Sheikh Abeid Amani Karume,imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa Amani na Utulivu,huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote wa Ndani au Nje.Amani iliyojengwa na imepelekea wageni,wakimbizi na watalii kuifanya Tanzania kuwa kivutio na kimbilio.
Tuendelee kuienzi na kuilinda Amani ya Nch yetu.Wapo wanaosema Kuwa Amani ni sawa na Yai mkononi,ukilivunja hautaweza kulinganisha kamwe;wengine wanasema kuwa Amani haina bei na ikipotea haina soko la kununu.Tuitunze Amani yetu.
Wilaya ya Serengeti itaadhimisha siku hii kwa kufanya maonyesho ya utalii kwenye viwanja vya Right to Play Mugumu.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti