• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Kiwavijeshi, Mdudu hatari kwa Zao la Mahindi

Imewekwa: February 13th, 2018

Na Simeon Nashon Waryuba.

Ni mdudu ambaye kwa kiingereza hujulikana kama Fall Armyworm au kwa jina la kitaalamu “Spodoptera frugipedra” asili yake ni Bara la America. Mdudu huyu alionekana kwa mara ya kwanza katika nchi za Africa Magharibi (Nigeria) mwishoni mwa mwaka 2016.

Hadi mwezi February 2017, kiwavijeshi huyu alikuwa ameshavamia nchi za Afrika Kusini, Kati na Mashariki zikiwemo Zimbabwe, Msumbiji, Zambia, Congo na Rwanda. Hapa nchini kiwavijeshi vamizi aliripotiwa kwa mara ya kwanza katika wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa mwezi Machi 2017.

Hadi mwezi Disemba 2017 kiwavijeshi huyu alisharipotiwa kwenye mikoa zaidi ya 15 Maarufu kwa kilimo cha mahindi ikiwemo Mbeya, Shinyanga,Ruvuma, Iringa, Geita, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro,Tanga, Kigoma, Kagera, Mwanza, Pwani na Lindi.

Mzunguko wa Maisha ya Kiwavijeshi vamizi {Fall Armyworm}

Ukuaji wa mdudu huyu hupitia katika hatua nne za ukuaji ambazo ni; yai – kiwavi – buu – mdudu kamili (nondo). Hatua ya kiwavi ndiyo inayoshambulia na kuathiri mazao.


Mazao yanayoshambuliwa na Kiwavijeshi vamizi (Fall Armyworm)

Kiwavijeshi ( Spodopter frugipedra) hushambulia aina nyingi za Mazao mfano nafaka (Mahindi, Mtama,Mpunga) Mikunde, mbogamboga, (nyanya, mchicha, matikiti, pilipili) ,mbegu za mafuta (karanga, alizeti,pamba) ,miwa, matunda, (migomba, miembe, michungwa) pamoja na malisho ya mifugo mf. Mabingobingo.

Kiwavijeshi vamizi hushambuliwa mazao katika hatua zote za ukuaji kwa mfano mahindi hushambuliwa yakiwa bado machanga hadi wakati yameshakomaa hivyo kufanya udhibiti kuwa ngumu na wa gharama kubwa.

Dalili za uharibifu wa Kiwavijeshi Vamizi kwenye zao la Mahindi.

  • Mdudu huyu hufanya uharibifu wa mazao akiwa katika hatua ya kiwavi (lava stage).
  • Hatua ya kwanza ya kiwavi (1st instar) hushambulia majani.
  • Majani ya Mahindi hutobolewa na kuacha matundu makubwa
  • Mabaki ya kinyesi kinachofanana na pumba huonekana juu ya majani ya mahindi
  • Viwavi huonekana kwenye magunzi, shina, na mbelewele

Wadudu wanavyoonekana katika sehemu ya mmea unapoota.

Mdudu akishambulia kwenye gunzi ka Mhindi

Jinsi ya Kudhibiti Kiwavijeshi Vamizi (Fall Armyworm)

Udhibiti wa kibaiolojia

Mdudu huyu anaweza kudhibitiwa kwa njia ya matumizi ya wadudu au viumbe marafiki kama vile Manyingu mf. Telenomus spp, Earwings, na Kuvu mf. Beauvera bassiana ,Bacillus thrugiensis n.k hata vivyo njia hii inahitaji maandalizi maalumu nap engine inaweza kuchukua muda mrefu kwa sababu ni lazima wadudu marafiki wawe wa kutosha.

Udhibiti Sango

  • Tumia mitego ya kuwanasa nondo ili kubaini mapema uwepo wa kiwavijeshi vamizi
  • Andaa shamba mapema na lima kwa kutifua ardhi ili mabuu (pupae) yaweze kukaushwa na Jua au kuliwa na ndege /wadudu wengine
  • Panda kwa wakati kwa kutumia mbegu na mbolea zilizoshauriwa na wataalamu kwenye eneo lako
  • Zingatia uzafi wa shamba kwa kuondoa magugu nyasi kuzunguka shamba na mabaki ya mazao ya msimu uliopita yanayoweza kuwa na masalia ya wadudu
  • Kagua shamba mara kwa mara n aondoa mimea inayoonyesha dalili za kushambuliwa.
  • Nyunyuzia majivu kwenye vikonyo ili kuua larva kwenye mimea iliyoshambuliwa
  • Tumia kilimo mchanganyiko wa zao la mahindi na jamii ya mikunde
  • Kilimo mzunguko kwa kubadilisha mazao jamii moja na nyingine
  • Epuka kusafirisha mimea/mazao kutoka shamba lililoathirika na Kiwavijeshi Vamizi

Udhibiti wa kutumia Viuatilifu

  • Kagua shamba kubaini uwepo wa lava wa Kiwavijeshi Vamizi kwenye shamba
  • Tumia viatilifu vilivyosajiliwa Tanzania kwa kufuata maelekezo kwenye kibandiko kilichopo kwenye kifungashio.
  • Kiuatilifu kipulizwe wakati wa asubuhi au jioni kwenye eneo lililoshambuliwa na Kiwavijeshi Vamizi
  • Kwa ushauri unaweza kutumia kiuatilifu chenye usajili wa jina la DUDUBA EC, Belt 480SC, Emamectin benzoate au Mupacron 50EC, DUDUALL, PROFECRON n.k
  • Viuatilifu vyote vina maelekezo ya jinsi ya kutumia lakini pia ni muhimu kuwasiliana na bwana/bibi shamba wa karibu na eneo lako kwa maelekezo zaidi.
  • Unapotumia viuatilifu jikinge vyema kwa mavazi sahihi na zingatia utunzaji wa mazingira.

Matumizi ya kiuatilifu iwe ni hatua ya mwisho baada ya mbinu nyingine kushindwa


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WASIMAMIZI PENDEKEZWA WA VITUO WATAKAOFANYA KAZI KATIKA ZOEZI LA UCHAGUZI MKUU TAREHE 29 OKTOBA, 2025. October 21, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. October 03, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA September 16, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI July 01, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AMTAKA MKANDARASI KUONGEZA NGUVU YA UTEKEKEZAJI WA MRADI WA MAJI SERENGETI.

    September 13, 2025
  • RC MTAMBI, AWAKARIBISHA WANANCHI KWENYE MAADHIMISHO YA MARA DAY.

    September 11, 2025
  • SEMINA YA SIKU TATU KWA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA JIMBO LA SERENGETI YAHITIMISHWA RASMI.

    August 06, 2025
  • BARAZA LA MAMLAKA YA MJI MDOGO SERENGETI LAZINDULIWA LEO.

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti