• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Mpango wa Kuinua Elimu - Tanzania (MKUE)

Start Date: 2015-07-01
End Date: 2020-06-30

Wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka Shule ya Msingi Mballibali wakiwa darasani

Idara ya elimu msingi ilianza kutekeleza Mradi wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE-T/EQUIP-T) tangu Juni, 2015. Kuanzia mwezi Januari, 2018 Halmashauri itanufaika na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi moja na choo cha matundu manne kutoka OR-TAMISEMI wakishirikiana na MKUE-T. Pia, shule mbili za Kebosongo, na Morotonga zitakamilishiwa maboma mawili ya vyumba vya madarasa kila shule. Kwa ujumla shughuli hii ya kukamilisha maboma na kujenga vyumba vyaa madarasa 18, ofisi 9 na matundu ya choo 36 itagharimu Tshs. 600,000,000/=

Shule zitakazo nufaika na ujenzi wa vyumba vya madarasa,ofisi na matundu ya choo manne ni shule shikizi za Manyago (Nyanungu), Bokore (Nyichoka), Maliwa (Nyiberekera), Korohongo (Mosongo), Nyangwe (Kwitete), Getarungu (Gesarya), Kegonga (Igina), Kwirengo (Bonchugu) na Gwikongo (Mbalibali).

Pamoja na shughuli hiyo itakayoanza Januari, 2018. Mradi wa MKUE-T/EQUIP-T umefanya shughuli zifuatazo tangu Juni, 2015 kwa lengo la kuinua ubora wa elimu Wilayani.

  • Kuwajengea uwezo walimu wakuu,walimu wakuu wasaidizi, wajumbe wa kamati za shule na Maafisa elimu Kata juu ya kuandaa mpango wa maendeleo wa shule(SDP)
  • Kuwajengea uwezo walimu wakuu, kamati za shule na Maafisa Elimu Kata juu ya majukumu yao ya uongozi na usimamizi wa shughuli za elimu shuleni
  • Kuwajengea uwezo Maafisa Elimu Kata kuhusu wajibu wao kama wadhibiti ubora/wakaguzi wa awali ngazi ya shule
  • Kutoa mafunzo ya mfumo wa taarifa za shule (SIS) kwa walimu wakuu,walimu wa TEHAMA shuleni na Maafisa Elimu Kata
  • Kuwajengea uwezo walimu wa darasa la kwanza na pili juu ya ufundishaji wa KUSOMA, KUANDIKA na KUHESABU (KKK) pamoja na kutoa mafunzo ya mapitio ya moduli “reflection” za KKK kila baada ya wiki 6
  • Kuwezesha uanzishaji wa vituo vya utayari (SRP)kabla ya kuanza darasa la kwanza katika maeneo yaliyo mbali (zaidi ya km 3) kutoka shuleni.
  • Mradi umeendesha mafunzo ya kuanzisha miradi midogo midogo ya kuiongezea shule kipato (income generation activities).
  • Mradi umetoa fedha kiasi cha Tshs. 825,000,000/= kwa shule 55 za msingi sawa na asilimia 50 ya shule zote Wilayani ili zianzishe miradi ya kuiongezea shule kipato (EK) na kupunguza utegemezi wa fedha kutoka serikalini, pia wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi waweze kuongeza ujuzi wa shughuli za uzalishaji na waweze kujitegemea wakiwa uraiani.
  • Mradi umetoa vishikwambi 139 kwa shule za msingi 109 na waratibu 30 kwa ajili ya kuboresha utoaji wa taarifa za shule kama mahudhurio, utoro, ufundishaji ,hali ya shule, uandikishaji na taarifa zingine muhimu
  • Mradi umetoa pikipiki 16 kwa Maafisa Elimu Kata sawa na asilimia 53, bado Kata 14 ambazo pikipiki zake zipo katika mchakato wa kuletwa, ili kuboresha usimamizi na ufuatiliaji ngazi ya Kata.
  • Mradi umeanzisha vituo vya utayari wa kuanza elimu ya sekondari (SSRP) ili kuwasaidia watoto wa kike kujenga msingi wa lugha ya Kingereza kabla ya kuanza kidato cha kwanza.
  • Mradi umeanzisha ushirikiano kati ya walimu na wazazi (UWW/PTP) ambao lengo lake ni kuimarisha ushirikiano kati ya shule na jamii, kuimarisha ufuatiliaji wa pamoja wa mwenendo wa mwanafunzi katika kujifunza baina ya walimu na wazazi na kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri pia, kufanya ukarabati mdogo mdogo katika miundombinu ya shule.
  • Mradi unatoa ruzuku ya UWW/PTP ya Tshs 550,000/= kwa shule 109  kwa mwaka sawa na Tshs. 59,950,000/=
  • Mradi unatoa ruzuku ya uendeshaji kwa Maafisa elimu Kata ya Tshs. Kati ya 150,000/= hadi 250,000/= kila mwezi, sawa na Tshs. 72,000,000/= kwa mwaka.

Mafanikio.

Kutokana na mchango huo wa MKUE-T/EQUIP-T Halmashauri imeweza kufanikiwa katika maeneo yafuatayo:

  • Kupunguza wanafunzi wasiojua KKK kutoka asilimia 19 hadi asilimia 5
  • Uongozi wa shule na kata umeimarika katika masuala ya utawala na uongozi wa shule
  • Ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 65.13 mwaka 2015 hadi asilimia 78.94 mwaka 2017
  • Ushiriki wa wazazi na jamii umeongezeka katika shughuli za maendeleo ya elimu, tumeweza kuongeza vyumba vya madarasa kutoka 748 mwaka 2015 hadi 839 mwaka 2017, nyumba za walimu kutoka 453 mwaka 2015 hadi 565 mwaka 2017, matundu ya choo kutoka 985 mwaka 2015 hadi 1143 mwaka 2017 na madawati kutoka 12,779 mwaka 2015 hadi 26,455 mwaka 2017.
  • Kuanzisha vituo vya shule shikizi kutoka vituo 0 mwaka 2015 hadi vituo 11 mwaka 2017
  • Kuimarisha ufuatiliaji, ukaguzi na usimamizi ngazi ya shule unaofanywa na Maafisa elimu Kata
  • Kuanzishwa kwa miradi midogo midogo ya kuziongezea shule kipato
  • Kuwajengea maarifa ya ufundishaji wa KKK, uandaaji wa Maandalio na Maazimio ya masomo pamoja na utengenezaji wa zana za kufundishia na kujifunzia walimu, walimu wakuu wa shule na Maafisa Elimu Kata.

Changamoto

Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto chache kama ifuatavyo:

  • Kata 14 hazina pikipiki hivyo kazi ya ufuatiliaji na usimamizi wa shughuli za elimu katani unakua ni ngumu.
  • Baadhi ya shule za msingi vishikwambi na soler zake havifanyi kazi ipasavyo kutokana na kuharibika na vingine mtandao kutoshika vizuri.
  • Ufuatiliaji wa shughuli umekuwa mgumu kwa ngazi ya Wilaya kutokana na kukosa fungu la ufuatiliaji.

Mkakati

  • Serikali kwa kushirikiana na MKUE-T washirikiane kuharakisha upatikanaji wa pikipiki 14 zilizobaki za Maafisa elimu kata
  • Vishikwambi na soler zisizofanyakazi ipasavyo zirekebishwe pamoja na pale ambapo mtandao haushiki vizuri wabadilishiwe line
  • MKUE-T wakishirikiana na OR-TAMISEMI waweke fungu kwa ajili ya shughuli za ufuatiliaji

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA January 02, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO WATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    April 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SERENGETI LAPITISHA BILIONI 48.8 KAMA MPANGO WA BAJETI YA HALMASHAURI 2025/2026.

    March 04, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI WILAYANI SERENGETI LAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA TARURA BILIONI 2.4

    March 03, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti