Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti leo 17/02/2021 imeendelea na zoezi la kugawa fedha kwa walengwa wa Kaya Masikini Tarafa ya Rogoro kwenye Vijiji vya Bisarara,Bonchugu,Mbirikili eyamburi na vijiji vingine vya jirani.
Zoezi limefanyika vizuri bila uwepo wa malalamiko yoyote kwani wanufaika katika vijiji wametembelewa na wawezeshaji akiwemo Mratibu wa Zoezi hilo la kugawa fedha hizo Bi Antusa Swai pamoja na Mshauri wa Tasaf Ndugu Sokoro Mnubi.
Katika Kijiji cha Nyamburi Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ndugu Jeremia Maro Gitano alithibitisha kuwa wamepokea Fedha Jumla ya Tsh 3,108,000/= kwa ajili ya kuzigawa kwa walengwa hao ambao wana jumla ya Idadi ya (51) ambapo alifanya mazungumzo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya Serengeti na kumthibitishia kuwa fedha zinatumika vizuri hasa kwa kundi la Wanawake ambao wamekuwa wakizitumia kwa shughuli mbali mbali kama Ufugaji,Kilimo pamoja na Biashara ndogo ndogo tofauti na Upande wa Wanaume ambao wao wakizipata huzitumia kunywea pombe za Kienyeji.
Baada ya maelezo hayo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamburi ndipo Mshauri wa Tasaf Ndugu Sokoro Mnubi alipata nafasi ya kuzungumza na wanufaika hao na kuwashauri juu ya matumizi mazuri ya fedha hizo na hasa katika kuzitumia fedha hizo pia kujiunga na Mfuko wa Afya wa CHF iliyoboreshwa ambayo inatolewa kwa Tsh 30,000/= ambayo pia wanafamilia wapatao (6) watapata Huduma za Matibabu katika Hospitali zote Nchini.
Imetolewa
Afisa Habari- Mahusiano
Emmanuel Isyaga Mwita
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti