Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe. Samson R. Wambura ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kisangura ,Imefanya Ziara ya Kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Matundu 12 ya vyoo vya wasichana katika Shule ya Sekondari Robanda yenye gharama ya Tshs.13,200,000/= zilizopokelewa Tarehe 28.12.2021 kutoka halmashauri ya wilaya ya Serengeti kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo.Pamoja na Mchango wa bati 17 zilitolewa na mbunge wa Jimbo la Serengeti Dkt.Amsabi Mrimi zimetumika kupaua vyoo hivyo.
Aidha Wananchi walileta viashiria vyenye thamani ya Tsh.8,450,000/= Mpaka sasa Mradi huo umekamilika.Uongozi wa Shule hiyo imeomba kujengewa matundu 10 ya vyoo vya wavulana ili kukidhi uwiano ulipo kutokana na ongezeko la wanafunzi.
Kamati imeipongeza shule kwa usimamizi mzuri wa mradi na kuichukua changamoto ya uitaji wa matundu mengine 10 kwa ajili ya vyoo vya wavulana.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti