ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UKAMILISHAJI WA MAABARA SHULE YA SEKONDARI MUSATI-KEBANCHABANCHA
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub Makuruma ambaye pia ni Diwani wa kata ya Busawe,imefanya Ziara ya Kutembelea na kukagua Mradi wa ukamilishaji wa Maabara Shule ya Sekondari Musati-Kebanchabancha.Shule ya Sekondari Musati ilipokea kiasi cha Tzs.30,000,000/= ikiwa ni kutoka katika Mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Maabara hiyo.’
Kamati imeridhishwa na na hatua za ujenzi wa Maabara hiyo,hivyo imeutaka uongozi wa shule hiyo kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi uweze kukamilika na kuwasaida wanafunzi
Aidha Kamati ilipata wasaa wakukagua Mradi wa ujenzi wa madarasa matatu fedha kutoka serikali kiasi cha Mil.60 ambapo ujenzi upo katika hatua ya msingi.Kamati imeutaka uongozi kusimamia ujenzi huo na kuhakikisha unaisha kwa wakati
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti