ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KENYANA -RING'WANI
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub Makuruma ambaye pia ni Diwani wa kata ya Busawe,imefanya Ziara ya Kutembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kenyana ambao ujenzi wake ulianza kutekelezwa Tangu 24.10.2022 baada ya kupokea kiasi cha Tsh.250,000,000/= zinazotokana na tozo.Fedha hizi zilikezwa kwenye kujenga Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD),Maabara,kichomea taka Majengo haya yapo katika hatua za ukamilishaji.Kwa awamu ya pili kituo hiki kilipokea kiasi cha Tzs. 250,000,000/=zinazotokana na Tozo zilizoelekeza Kujenga Jengo la Upasuaji linaloungana na wodi ya wazazi ,Jengo la kufulia na Njia ya Kuunganisha Majengo yote,Majengo hayo yamefikia hatua za Boma na ujenzi unaendelea.
Kamati imeridhishwa na Ujenzi huo na kuutaka uongozi wa kata na kituo kusimamia ujenzi huo na kuhakikisha unaisha kwa wakati.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti