WATUMISHI IDARA YA AFYA WATAKIWA KUZITUNZA PIKIPIKI WALIZOKABIDHIWA
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub M.Makuruma kwa niaba ya uongozi na menejimenti ya halmashauri ya wilaya ya Serengeti amewataka watumishi wa idara ya afya ,Ustawi wa jamii na Lishe kuzitunza pikipiki walizokabidhiwa leo tarehe 02.novemba 2022 ili ziweze kudumu na kutekeleza majukumu yalikusudiwa.
Mhe.Makuruma ameyasema hayo katika tukio fupi ya kuwakabidhi Pikipiki tatu aina ya boxer watumishi hao wanaoshughulika na kutoa huduma za Mama na mtoto,Lishe na ustawi wa Jamii.
‘’Vyombo hivi I rasmi kwa ajili ya kazi ya kuwahudumia wananchi,Rai yangu pikipiki hizi zitunzwe ili ziweze kutusaidia sawa sawa na Matakwa ya serikali,Haiwezekani baada ya siku mbili au tatu chombo kipo juu ya mawe,bahati nzuri tumepewa pikipiki ambazo ni imara aina ya Boxer’’amesema makuruma.
Aidha Mhe.Makuruma amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuikumbuka wilaya ya Serengeti kwa kuleta miradi mbalimbali na vitendea kazi.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Ndg.Kivuma Msangi amemshukuru Rais samia kwa wilaya ya Serengeti kuwa sehemu ya mgao wa kupata pikipiki hizo,amewasisitiza watumishi waliopata pikipiki hizo kuzitunza.
Nao watumishi waliopata pikipiki hizo wameishukuru serikali kwa kuwarahisishia majukumu yao na kuahidi kuzitunza na kuzifanyia majukumu yaliyokusudiwa.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti