Wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu halmashauri ya Wilaya ya Serengeti wametakiwa kutumia mikopo hiyo kujiinua kiuchumi kama lilivyo lengo la Serikali na si kuitumia kufanya starehe kwani kufanya hivyo watashindwa kurejesha mikopo hiyo.
Akizungumza na wanufaika wa mikopo hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Kemirembe Lwota amesema lengo la Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha inawainua wananchi wake kiuchumi hivyo uwepo wa mikopo ya asilimia 10 utumike kutimiza azma ya Serikali katika kuwapa maisha bora wananchi huku akisisitiza wanufaika hao kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
"Msigawane fedha hizi Kwa matumizi yenu binafsi bali zitumieni kulingana na maandiko mradi yenu, na nyie ambao mmefanikiwa kupata mikopo hii onesheni kwa vitendo kuwa mikopo hii inamanufaa na boresheni maisha yenu kupitia biashara". Alisema Mhe. Kemirembe.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ndg. Mujibu Babara amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kukumbuka viapo walivyoapa wakati wa kuchukua mikopo hiyo huku akiwataka kuzingatia nidhamu ya fedha ili waweze kurejesha kwa wakati mikopo hiyo kama kanuni zinavyosema.
"Bila nyingi kurejesha hakuna namna ambayo wengine wataweza kukopeshwa, hivyo rejeaheni ili wengine waweze kukopeshwa" alisema Babara.
Nao baadhi ya wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 wameishukuru Serikali ya awamu ya Sita Kwa kurudisha mikopo hii huku wakiaidi kutumia fedha hizo kujiinua kiuchumi kwa kufanya biashara zenye tija jambo litakalowawezesha kurejesha mikopo hiyo Kwa wakati.
Kwa awamu ya kwanza ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imetenga kiasi cha shikingi milioni 360,000,000/= ambapo Vikundi 53 vimenufaika na fedha hizo za awamu ya kwanza ya utoaji wa mikopo hiyo ambayo haina riba.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti