Wananchi wilayani Serengeti wameendeela kuelimishwa na kutakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita vitendo vyote vya kikatili vinavyofanyika katika jamii zikiwemo ndoa za utotoni ,ukeketaji Ikiwa ni siku 16 za kupinga vitendo vya kikatili nchini Tanzania iliyoanza kuanzia tarehe 25 Novemba hadi 10 disemba 2022.
Akizungumza wakati wa utoaji wa mafunzo hayo kwa walengwa wa TASAF waliojiotokeza afisa maendeleo ya jami wilaya ya Serengeti Bi. Josepha Gurti amewasisitiza wananchi hao kuwa mstari wa mbele katika kutoa tarifa katika vyombo vya usalama watapoona au kusikia vitendo vya kikatili vinavyoendelea katika Jamii ili kuondokana kabisa na vitendo hivyo vya kikatili ambavyo vimekuwa na athari kubwa kwa wanaotendewa haswa watoto wa kike.
Mwaka huu ni mwaka wa ukeketaji katika wilaya ya serengeti na mengine wawezezaaji wametumia warsha hiyo kuwataka wananchi hao kutojihusisha na vitendo hivyo vya ukeketaji sambamba na kutoa taarifa iwapo vitendo hivyo vitafanyika ili hatua za kiusalama ziweze kuchukulia.
Pia wanufaika hao wa mpango wa TASAF Wameendelea kukumbushwa kuwa na namba za NIDA ili kuwasaidia akupokea ruzuku zao kwa njia za kimtandao ambao ni njia iliyodhibitika kuwa bora na salama Zaidi,Wanufaika hao pia wamefundishwa kuhusu ajira za muda ambazo zitawasaidia kujikomboa kiuchumi.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti