Kamati ya Jumuiya ya Tawala za mitaa (ALAT) Mkoa wa Mara wametembelea na Kukagua Mradi wa Ujenzi wa Tanki la Kuvunia na kuhifadhia Maji la Lita elfu kumi katika machinjio ya Mugumu wilayani Serengeti.
Mradi huu Ni miongoni mwa miradi iliyopangwa kutekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti kupitia Idara ya mifugo na uvuvi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa kutumia mapato ya ndani.
Mradi huu ulitengewa Kiasi Cha Tsh.8,220,000/= ambapo hadi sasa umetumia kiasi cha Tsh.7,925,524.8/= Mradi na umekamilika na upo tayari kutumika.kiasi kilichobaki ni Tsh.294,475.2/=
Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 09.04.2022 shughuli mbalimbali ziliweza kufanyika kuanzia kuanza hadi kukamilika kwa mradi huu,ikiwemo uchaguzi wa eneo la mradi.
Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Mara Mhe.Daniel kamote ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwa kupeleka 40% kwenye miradi ukiwemo mradi wa wa ujenzi wa tanki la kuvunia na kuhifadhia maji katika manjio ya Mugumu.,Pia amempongeza afisa mifugo wilaya ya Serengeti Bi.Rehema Koka kwa ubunifu wa uibuaji wa Mradi huu pamoja usimamizi wa mradi huo.
‘’Machinjio na maji na vitu ambavyo haviwezi kutengana,endeleni kuhakikisha usafi katika eneo maeneo haya,hata mimi nimejifunza kitu na mradi huu ni mfano wa kuigwa ‘’alisema Mhe.Chomote
Uwepo wa Mradi huu utasaidia upatikanaji wa maji ya uhakika katika machinjio hii pamoja na kuimarika kwa usafi katika eneo hili la machinjio hivyo kuepuka mlipuko wa magonjwa na adha mbalimbali.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti