Wadau wa zao la tumbaku Mkoani Mara wametakiwa kuzingatia kikamilifu miongozo na kanuni za kilimo cha zao hilo ili kufikia lengo la kuongeza uzalishaji na kuboresha hali ya wakulima wa zao hilo.
Hayo yamezungumzwa Leo Jumanne 17,2025 na Mkuu wa Wilaya ya Rorya Dkt. Khalfan Haule, wakati akizungumza katika mkutano wa kwanza wa wadau wa zao la tumbaku uliowaleta pamoja wakulima, wanunuzi, wawakilishi wa serikali, na taasisi za kifedha kwa lengo la kuboresha uzalishaji, masoko, na ustawi wa wakulima wa zao hilo katika kutafuta suluhu ya changamoto zinazokabili sekta ya kilimo cha tumbaku katika Mkoa wa Mara uliofanyika katika ukumbi wa Kisare Wilayani Serengeti.
Akizungumza katika mkutano huo Dkt. Haule amesisitiza kuwa mafanikio katika sekta ya tumbaku yanategemea sana kufuata taratibu za ulimaji na uvunaji wa zao hilo ili kuleta manufaa makubwa kama ilivyokusudiwa.
"Serikali imeweka fedha nyingi kataka ruzuku ya zao hili hivyo ni muhimu sana kwetu kuhakikisha tunasimamia miongozo ya kitaalamu ya kilimo cha tumbaku Kuanzia upandaji, utunzaji, uvunaji, hadi ukaushaji, kila hatua inahitaji umakini ili kupata tumbaku yenye ubora inayokidhi viwango vya masoko ya ndani na nje." alisema Dkt. Haule
Ameongeza kuwa kuzingatia kanuni hizo kutasaidia kuepusha hasara, kupunguza magonjwa ya mimea, na hatimaye kuongeza mavuno kwa ekari, jambo litakalowezesha wakulima kunufaika zaidi na jasho lao huku akipiga vikaoi tabia ya utoroshaji wa tumbaku kuelekea nchi jirani
Aidha Dkt. Haule amewataka wanunuzi wa tumbaku na taasisi zinazotoa pembejeo kuhakikisha wanatoa elimu sahihi na endelevu kwa wakulima.
Awali akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa bodi ya tumbaku mkoa wa Mara Ndg. Momanyi Range ameomba ushirikiano baina ya serikali, wakulima na wataalam ili zao la tumbaku liweze kuwa na tija na pande zote.
Mkutano wa wadau wa zao la tumbaku umehudhuriwa na wawakilishi kutoka bodi ya tumbaku, benki mbalimbali, viongozi wa wilaya zote za Mkoa wa Mara zinazolima tumbaku, na wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti