Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inayo fedha kiasi cha bilioni sita za kitanzania katika ujenzi wa daraja la mto mara linalojengwa katika mpaka wa Wilaya ya Serengeti na Tarime.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mheshimiwa Marwa Ryoba Mara baada ya kuwasili Wilayani Serengeti akitokea Wilaya ya Tarime
Mheshimiwa Majaliwa amsema hayo leo tarehe 18 januari 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mara alipokuwa anaingia katika Wilaya ya Serengeti akitokea Wilaya ya Tarime ambako Mto Mara hutenganisha Wilaya hizo.
“Tunatarajia ifikapo mwezi wa tatu mwaka huu (2018) daraja hili litakuwa limeshakamilika hivyo kurahishisha huduma za mawasiliano kati ya wilaya hizi kwa ufanisi zaidi "alisema Mheshimiwa Majaliwa.
Kukamilika kwa daraja hilo lililoanza kujengwa mwezi wa tatu (3) mwaka 2017 na mkandarasi Gemen Engineering kunaashiria ujio wa barabara ya lami kutoka Tarime mpaka Mji wa Mugumu Serengeti na kuondoka kero ya muda mrefu ya wakazi wa Mji wa Mugumu Serengeti wanaokosa huduma muhimu ya mawasilano ya barabara ya lami inayounganisha na Wilaya hiyo na zingine.
Mheshimiwa Majaliwa alisema kuwa baada ya ujenzi wa daraja kukamilika, serikali itaanza mara moja mchakato wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka tarime mpaka Mji wa Mugumu. Waziri Mkuu hakusita kuzungumzia kero ya muda mrefu juu ya barabara ya lami inayounganisha Mkoa wa Mara na Arusha kupitia Wilaya ya Serengeti na Ngorongoro na kusema “kwa muda mrefu sasa serikali imekuwa katika mazungumzo na wadau wa maendeleo wa kimataiafa juu ya ujenzi wa barabara ya lami katika hifahdi ya taifa ya Serengeti ambayo ni miongoni wa vivutio vya dunia na kulingana na makubaliano tuliyowekeana bado ipo changamoto katika fumbuzi wa jambo hili” alisema Mheshimiwa Majaliwa na kuwataka wananchi kuwa na subira wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa jambo hilo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mheshimiwa Juma Porini wakati anawasili katika Wilaya ya Serengeti akitokea Wilaya ya Tarime.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhandisi Juma Hamsini wakati akiwasili Wilaya ya Serengeti akitokea Wilaya ya Tarime.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti