SERIKALI imetenga zaidi ya Bilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi uwanja wa ndege wa Serengeti mkoani Mara ambapo kukamilika kwake kunatajwa kukuza uchumi wa Wakazi wa Serengeti.
Hayo yamebainishwa jana Jijini Dar es Salaam wakati utiaji saini baina Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini(TAA) na Kampuni ya Saba Engineering Private Campany kwa ajili ya upembuzi yakinifu juu ya uwanja huo.
Akizungumzia Mkataba huo,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini(TAA),Abdul Mambokaleo,amesema mkataba huo wa miezi sita na kampuni hiyo itatoa ushauri n.
“Hawa wapewa miezi sita baada ya miezi sita kandarasi kukamilika watakuja na mapendekezo ya jinsi ya kujenga uwanja huu”Amesema
Mkurugenzi amesema lengo la serikali kujenga uwanja huo ni kusaidia kukuza sekta ya utalii katika mbuga za serengeti.
Kwa Upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti,Dkt . Maulid Suleiman Madeni,ameipongeza TAA kwa hatua ya kuanza ujenzi wa uwanja huo na kusema utakuwa mkombozi kwa wakazi wa eneo hilo.
Amesema wananchi wa Serengeti wategemee kupata makubwa kutokana na kukua kwa Shughuli za uchumi zitakazotokana na ujenzi wa uwanja huo.
“Watalii wote walioshuka Arusha sahivi watashuka Serengeti na baada ya uwanja huu kukamilika ndege zaidi mia moja siku za kilele zitashuka Serengeti maana hapa uchumi utaanza kukua eneo hili”
Dkt Madeni amesema uwanja huo utapelekea ofisi mbalimbali kujengwa zitapelekea watu kupata Ajira na kusaidia kujiingizia kipato.
Hata hivyo,Dkt Madeni amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake kutoa fedha uwanja wa ndege wa Serengeti.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti