Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetoa mkopo usio na riba yenye kiasi cha Tsh. Milioni 136,374,130/- kwa vikundi 28 vya wanawake,vijana na watu wenye walemavu ikiwa ni mkopowa wa asilimia 10% za makusanyo kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mfano ,Mhe.Ayubu Makuruma , Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti ametoa wito kwa vikundi hivyo kutumia fursa ya mikopo isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri ili kujikwamua kiuchumi ambapo amesisitiza vikundi hivyo kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuendelea kunufaika zadi na kutoa wigo wa utoaji wa mikopo kwa wananchi wengine.
‘Natoa wito kwenu baada ya kupata mkopo huu fanyeni kazi kwa bidi ili mjikwamue kiuchumi sambamba na kurejesha kwa wakati kwa mujibu wa utaratibu kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wasio fanya marejesho na kukwamisha wananchi wengine kunufaika ‘’amesema Makuruma.
Katibu tawala wa wilaya ya Serengeti Ndg.Qamara C.Qamara kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Serengeti amevisisitiza vikundi vilivyonufaika na mkopo huo kutumia mkopo huo kwa malengo na shughuli zilizokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi.
‘’Niwasihi mzingatie yote tuliyowaasa,Nendeni Mkaweke juhudi kulingana na malengo ya vikundi vyenu tunataka tuone tija’’amehimiza Qamara.
Mwakilishi wa meneja wa Benki ya NMB Bi.Beatrice Kamugisha ametoa wito kwa vikundi kuzitumia pesa hizo vizuri kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla lakini pia kujiwekea akiba .
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Serengeti Ndg.Kivuma H.Msangi amevipongeza vikundi vya wanawake kwa kuwa mstari wa mbele katika kurejesha mikopo hiyo na kuvitaka vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu kuongeza juhudi katika urejeshaji wa mikopo sambamba na kufuata taratibu stahiki wakati urejesha wa mikopo hiyo.
Naye Katibu wa mbunge Ndg. Julius Anthony kwa niaba ya Mbunge amehimiza vikundi vilivyonufaika kuendelea kukuza mitaji kwa kujikita katika shughuli mbalimbali za kiuchumi pia ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwa juhudi kubwa ya ukusanyaji wa mapato na utoaji wa asimilia 10% kwenye vikundi.
Awali akisoma taarifa kwa Mgeni Rasmi afisa wa Maendeleo ya Jamii kwa niaba ya mkuu wa Idara hiyo Bi.Neema Msuya amesema mkopo huo Milioni 136,374,130/- ni muendelezo wa utoaji wa mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri ambapo mkopo wa
million. 152,460,000/- kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Kupitia mkopo huo vikundi 17 vya wanawake,vinane (8) na vitatu (3) vya watu wenye ulemavu vilinufaika na mkopo huo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wakuu wa idara na vitengo, na watumishi wa idara ya maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti