Baraza la Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya serengeti Mkoani Mara Limejipanga kukusanya zaidi ya shlingi Bilioni 39,kutoka vyanzo mbalimbali vya Mapato.
Kaimu afisa Mipango wa halmashauri hiyo GEORGE KIHAMBA akisoma makisio hayo amesema msimu uliopita halmashuri hiyo ilipanga kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni 42 lakini kutokana na changamoto mbalimbali haikufikia lengo
Katika kikao hicho Mwenyekiti wa halmashuri hiyo AYUBU MAKURUMA amewakata Madiwani kusaidia watendaji wa halmashauri kukusanya Mapato ambayo yanakuwa msaada katika kuendelea shughuli mbalimbali za Maendeleo katika kata zao
kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoani Mara VICTOR RUTONESHA amelieleza Baraza la Madiwani katika halmashauri hiyo kuwa mpango wa ujenzi wa uwanja wa Ndege katika halmashauri hiyo upo pale pale licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo ambazo bado zinatafutiwa ufumbuzi.
aidha Madiwani katika halmasahuri ya wilaya ya Serengeti Mkoani Mara wameombwa kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani humo katika miradi mbalimbali ya Maendeleo,Mkuu wa TAKUKURU katika wilaya hiyo JULIUS MSOKA ameyasema hayo katika baraza la Madiwani huku akitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa wawikilishi hao wa Wananchi lakini pia akikabidhi Mpango wa taasisi hiyo ujulikanao kama TAKUKURU-RAFIKI
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti