Kuelekea kilele cha siku ya wazee Duniani ambayo huadhimishwa kila Oktoba Mosi ya Kila Mwaka,Wilaya ya Serengeti imeadhimisha kwa kutoa elimu ya ustawi na afya kwa wazee katika Kata ya mbalimbali,Wazee wameombwa kuwa chachu ya mabadiliko na upingaji wa vitendo vya kikatili katika maeneo yao.
Akizungumza na wazee hao Afisa ustawi wa Jamii Bi.Judith Petro,amewataka wazee hao kutambua kuwa serikali ina wathamini na kuwajali ndo maana imetenga siku hii muhimu kwa ajili ya kukaa nao na kuzungumza nao mambo mbalimbali yakiwemo ya afya na ustawi.
‘’Sera iliwekwa kukaa na wazee na kuzungumza nao Taifa linaamini kwamba bila wazee tusingekuwa hapa,wazee wametutoa mbali kiuchumi,kiutamaduni,kijamii’’alisema Bi.Judy
Kwa niaba ya wazee wengine wa wilaya ya Serengeti ,wazee wa mbalibali walipata elimu ya afya juu ya maswala mbalimbali ya ustawi na afya,afisa ustawi kutoka ofisi ya ustawi wa jamii bi.Mwajuma Machoki aliwasihi kuwa mstari wa mbele katika kupinga na kuzuia vitendo vyote vya ukatili vinavyotokea katika familia na jamii kwa kuwa wazee ni chachu ya mabadiliko chanya katika Jamii zao.
‘’Ukatili upo unaondeka katika jamii na maeneo yetu kuanzia ngazi ya familia na kwa jamii nzima ,ikiwemo swala la kupiga,ukekeataji .ukatili wa kingono, na hivyo kufanya watoto kukimbia makazi yao,na hii ni kutokana na wazee kufanyiwa hivyo na kutaka watoto wao na wajukuu kufanyiwa hivyo,’’alisema Bi.Mwajuma
Aliendelea kwa kuongeza kuwa ni muhimu wazee kutazama kwa ukaribu ukatli wa kiuchumi ambao watoto wanafanyiwa haswa katika ugawanya sawa wa rasilimali zilizopo.
Sambamba na hayo wazee pia wamekumbushwa kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko haswa ugonjwa wa Ebola ambao umetokea Nchi jirani ya Uganda,lakini pia wazee hao walipata elimu ya afya ya macho,kinywa na meno na kufanyiwa uchunguzi.
Siku hii ya wazee duniani imebebwa na kauli mbiu i‘’ustahimilivu na mchango wa wazee ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa’’
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti