Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Ally S.Hapi, Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kupata Hati safi ya Mkaguzi mkuu wa Serikali 2020/2021, katika baraza maalumu la kupitia Hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG.
RC Hapi amewapongeza Waheshimiwa madiwani,wataalamu na uongozi mzima wa Halmashauri ya wilaya Serengeti kwa jitihada na weledi wa kusimamia vyema miradi inayoletwa na serikali,lakini pia kutokuwepo kwa migogoro ambayo inangeweza kupelekea kukwama kwa miradi hiyo.
Aidha ,amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Ndg.Kivuma H.Msangi pamoja jopo lake la wataalamu kwa kusimamia vyema zoezi la ukusanyaji wa Mapato2021/2022 ambapo ukusanyaji umefikia 92% .
Mhe.Hapi amewaomba waheshimiwa Madiwani kusimama kidete katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ili mapato hayo yaweze kusaidia kuleta maendeleo kwa Wananchi.
Mkuu wa Mkoa amewataka watumishi,wakuu wa idara na Vitengo kuwajibika katika nafasi zao kusimamia vyema miradi inayoletwa na serikali na kuzungumza na wananchi wakati wa kutembelea miradi hiyo kuweza kupata maoni ,aidha kuacha mara moja tabia ya kukaa ofisini.
RC Hapi amesisitiza Halmashauri kuwekeza Nguvu Zaidi katika kukusanya Mapato Zaidi haswa yKatika mahoteli yaliyopo Mbugani,wadeni ambao hawajalipa madeni na kuwafikisha katika vyombo vya dola wote watakaokwamisha au kukaidi.
Mwisho,Mhe.Hapi amegiza uongozi wa Wilaya kuhakikisha inafuta hoja zote zilizobainishwa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt.Vincent Mashinji amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa ziara hiyo na kumuahidi kusimamia maagizo yote aliyayatoa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub Makuruma, amempongeza RC Hapi kwa kazi kubwa anayoifanya katika Mkoa wa Mara na kumtoa hofu juu ya miradi yote inayoletwa na iliyopo kuwa itasimimiwa kikamilifu na kwa weledi mkubwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti