Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani ametoa zawadi za chakula kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi kwa Shirika la Hope for girls and women in Tanzania lilipo wilayani Serengeti Mkoa wa Mara,likiwa ni Miongoni mwa shirika yanayopambana dhidi ya vitendo vya Ukatili na unyanyasi wa Kijinsia.
Akikabidhi Zawadi hizo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleimani Mzee, Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Vincent Mashinji amemshukuru Rais Samia kwa kutoa zawadi hizo za chakula katika wilaya ya Serengeti katika kituo cha hope.
Dkt.Mashinji amekipongeza kituo hicho salama kwa juhudi kubwa ya kuwalea watoto waliokimbia vitendo vya ukeketaji na ukatili wa kinjisia ,amewataka viongozi wa kisiasa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo hivyo .
Aidha,Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Serengeti Ndg.Gasper Irigo ameungana na viongozi wengine Kumshukuru Rais samia na kuahidi kushirikiana kwa ukaribu na vituo vyote vinavyolelea watoto yatima,wenye mazingira magumu na waliokimbia vitendo vya ukatili na unyanyasi.
Nae, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Serengeti ameitaka jamii kwatunza watoto ili waweze kutimiza ndoto zao na kuiomba serikali kuzidi kupambana na wote wanaofanya vitendo vya kikatili na vya unyanyasi wa kijinsia hatua kali ziendelee kuchukuliwa dhidi yao.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa kituo hicho Rhobi Samweli amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa zawadi kubwa ya chakula kwa ajili ya watoto wa kituo hicho wapatao 90 waliokimbia na kukutwa na matukio mbalimbali yakiwemo ukeketaji,vipigo,ndoa za utotoni,ubakaji na manyayaso na ameiomba serikali kuzidi kuwashika Mkono na kutunga sharia kali za kumlinda mtoto wa kike.
Huu ni Muendeleo wa Rais samia kuwagusa watoto wote nchini Tanzania wenye mahitaji ya chakula hii ni katika kusherehekea Sikukuu ya Krismasi inayoadhimishwa tarehe 25 disemba 2022 duniani kote.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti