Kamati ya afya ya Msingi (PHC) wilayani Serengeti imejiwekea mikakati mbalimbali ya kupambana na magonjwa ya milipuko ikiwemo ebola na uviko 19 ili kuifanya jamii kuwa salama,mikakati hiyo ni pamoja na kutoa elimu na hamasa Kwa jamii juu ya kujikinga na magonjwa ya milipuko,kuwepo kwa matangazo ya kujikinga na magonjwa kwa njia za vyombo vya muziki,uhamasishaji wa nyumba kwa nyumba kwa nyumba kwa kutumia wapiga mbiu pamoja na utambuzi wa walengwa wasio chanja chanjo ya uviko 19 kwa kila eneo la huduma kwa kila kituo cha kutolea huduma.
Akifungua kikao hicho cha kamati ya afya ya msingi Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Vincet mashinji ameitaka jamii kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa ebola na uviko 19 kwa kupata chanjo ya uviko 19 pamoja na kukamilisha chanjo kwa wale ambao hawajamaliza dozi chanjo ambayo inapatikana katika vituo vya kutolea huduma lakini pia kwa kampeni ya siku ya 10 ya kutembea nyumba kwa nyumba kutoa chanjo hii kuanzia tarehe 24.10.2022 .Pamoja kuepuka mizoga ya wanyama na kuwa muingiliano nao wa karibu.
Katika kukamilisha idadi ya walengwa wa kuchanjwa chanjo ya uviko 19 ambayo ni asilimi 70 ya walengwa, wote idara ya afya imeaanda kampeni ya uchanjaji ya siku 10 katika kata zote 30 za wilaya ya Serengeti .
Mganga Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Emiliana Donald ameiomba Jamii kujitokeza ili kupata chanjo hiyo ya uvikp 19,ambayo itatolewa nyumba kwa nyumba sambamba na kuchukua tahadhari zote ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kwa kutumia vitakasa mikono.
Nae Mratibu wa chanjo wilaya amesema ‘’tunatoa wito wa jamii kwa ambae ajapata chanjo hii ya uviko 19 ajitokeze apate chanjo hii na wale ambao hawajakamilisha dozi wajitokeze kukamilisha dozi ili kuwa na kinga kamili dhidi ya ungojwa huu’’
Kampeni hii inalenga kuinua kiwango cha uchanjaji kutoka asimilia 39.7 ambayo wilaya imefikia mpaka mpaka asilimi 70 ya uchanjaji.AMREF,Red Cross na WFP ni miongoni mwa Mashirika yatakayokuwa bega kwa bega na wilaya ya Serengeti katika kuhakikisha lengo linafikiwa .
Kutokana na kusamba kwa ugonjwa wa Ebola kamati imeshauri jamii kupunguza safari zisiza lazima kwenda katika maeneo ugonjwa huu wa ebola upo hususa ni Uganda lakini jamii imeshauriwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa mbalimbali.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti