Na.
Goodluck Mwihava
Serengeti-Mara
Mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Serengeti Mkoani Mara zimesababisha uharibifu wa Miundombinu ikiwemo shule,kituo cha afya na Makazi ya Watu.
Mvua hiyo iliyoambata na upepo Mkali imeezua Paa za shule ya Msingi Nattabigo pamoja Paa katika stoo na jiko katika nyumba ya walimu,lakini pia kuangusha miti katika Maeneo mbalimbali,Kituo cha afya Natta ni Miongoni mwa Tasisi iliyoathiriwa na Mvua hiyo kwa kuanguka kwa miti iliyoangukia Jengo na kusababisha nyufa na kuharibika kwa kichomea taka.Upande wa makazi baadhi ya nyumba paa zimeezuliwa na miti kuangushwa.
Akizungumza wakati wa ziara ya kuwatembelea wahanga na Tasisi ambazo miundombinu imeharibiwa
Mkuu wa wilaya serengeti Dkt. Vincent Mashinji amewapa Pole waliopata athari hizo na kuwaasisitiza kupanda miti,lakini pia kuhakikisha kila Mwanafunzi ana Mti ili kuzuia athari kubwa zaidi kwa baadae
Aidha kwa upande wa serikali itafanya tathimini na kuhakikisha kila Kitu rudi kwenye hali yake
Diwani wa Kata ya Natta Mhe. Porini
Ameushukuru uongozi wilaya kwa kufika katika Eneo hilo na kuhakikishia uongozi watasimamia kwa ukaribu marekebisho na athari zote zilizojitokeza ili huduma kwa wananchi ziweze kuendelea.
Nae Mtendaji Kata ya Natta Bw.Sagenda Bomani amewahakikishia wananchi ofisi yake itashirikina nao bega kwa bega.
Kaimu mwalimu mkuu shule ya msingi Mwl.Madirisha amelezea tukio ilo na kuomba msaada wa haraka ili masomo yaweze kuendelea .Mganga mfawidhi kituo cha afya Natta Dkt.JUMA KIPINGU amekiri kutokea na tatizo hilo na kuomba jitihada za haraka zifanyike ilinkurudisha huduma katika hali ya kawaida
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti