Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti leo 19/02/2021 imekamilisha zoezi la uwasilishaji fedha kwa walengwa wa Kaya Masikini Tarafa ya Ngoreme kwenye Vijiji vya Nyamihuru,Nyamakobiti, Messaga, Nyagasense, Remung’orori na Msati.
Zoezi limefanyika vizuri bila uwepo wa malalamiko yoyote kwani wanufaika wote katika vijiji ambavyo vimetembelewa na wawezeshaji akiwemo Mshauri wa Tasaf Ndugu Sokoro Mnubi wamethibitisha kwamba zoezi limeenda vizuri bila malalamiko ya aina yoyote.
Katika Kijiji cha Nyamihuru Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bi Happy Fanuel Mwita alithibitisha kuwa wamepokea Fedha Jumla ya Tsh 3,030,000/= kwa ajili ya kuzigawa kwa walengwa hao ambao jumla ya Idadi yao ni (49) ambapo alifanya mazungumzo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya Serengeti na kumthibitishia kuwa fedha zinatumika vizuri hasa kwa kundi la Wanawake ambao wamekuwa wakizitumia kwa shughuli mbali mbali kama Ufugaji,Kilimo pamoja na Biashara lakini pia Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndugu David Chacha Mgendi.
Happy Fanuel Afisa Mtendaji aliesimamia zoezi akiwa na Muwezeshaji Bwana Nyambita
Baada ya maelezo hayo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamehuru na Mwenyekiti wa Kijiji hicho ndipo Mshauri wa Tasaf Ndugu Sokoro Mnubi alipata nafasi ya kuzungumza na wanufaika hao na kuwashauri juu ya matumizi mazuri ya fedha hizo na hasa katika kuzitumia fedha hizo pia kujiunga na Mfuko wa Afya wa CHF iliyoboreshwa ambayo inatolewa kwa Tsh 30,000/=.
Davidi Chacha Mgendi Mwenyekiti Kijiji cha Nyamihuru
Ziara hio iliendelea mpaka katika Kijiji cha Nyagasense ambapo Mshauri wa Tasaf Ndugu Sokoro Mnubi alipokelewa na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ndugu Mahitari Hunda pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndugu Matiko Daniel Ngerecha ambao pia walithibitisha kwamba zoezi linaenda vizuri na ndio walikuwa wanakamilisha zoezi Majira ya Saa 7:38 Mchana ambapo pia alipata nafasi ya kuelezea changamoto za Mradi huo kwani walengwa ambao wanatokana na kundi la Wanaume wengi wao huzitumia vibaya Fedha hizo kwa kunywa pombe na tayari Serikali ya Kijiji imeshawaita na kuwaonya ili waweze kuacha tabia hizo lakini pia akachukua nafasi hio kuwapongeza kundi la akina Mama kwa matumizi mazuri ya fedha hizo ambazo zimewasaidia kujenga nyumba na kuanzisha biashara ndogondogo ambazo kwa sasa zinasaidia kuendesha familia zao.
Katika Kijiji cha Msati Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Msati Ndugu Mafuru Sagati amethibitisha kuwa wamepokea Fedha kiasi cha Tsh 3,048,000/= ambazo zimewasilishwa vizuri bila kuwepo kwa malalamiko yoyote ambapo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndugu Mwita Daudi Mgendi amethibitisha kuwa fedha hizo zinatumiwa vizuri na walengwa hasa kwenye shughuli za Maendeleo.
Mafuru Sagati Afisa Mtendaji Kijiji cha Msati
Kijiji cha Remung’orori kimepokea fedha kiasi cha Tsh 2,412,000/= Afisa Mtendaji wa Kata Ndugu Geofrey Innocent Mzee ambaye ndie amesimamia zoezi hilo amethibitisha kuwa fedha hizo kwa Kjiji cha Remung’orori zinatumika vizuri na hakuna shida yoyote na kwamba wanufaika 48 kwa sasa ndio wanapokea fedha hizo.
Geofrey Innocent Mzee Afisa Mtendaji Kata Magange aliesimamia zoezi
Imetolewa
Afisa Habari- Mahusiano
Emmanuel Isyaga Mwita
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti