Ujenzi wa mradi wa maji wa RUWASA katika kijiji cha Nyiberekera wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.2 ulioanza kutekelezwa mwezi Machi 2023 wawekewa jiwe la msingi na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023.
akiweka jiwe la msingi katika Mradi huo Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu Ndg. Abdala Shaibu Kaimu amefurahishwa na usimamizi mzuri wa Mradi huo chini ya RUWASA na kuwataka kuendelea kusimamia vyema Mradi huo mpaka kukamilika kwake ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi baadhi ya maelekezo madogomadogo ili kuongeza ubora zaidi wa Mradi huo.
Aidha kukamilika kwa ujenzi wa mradi huu kunategemewa kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kutoka asilimia 25 iliyopo hivi sasa na kufikia asilimia 100 ya watu wote 6,708 wa kijiji cha Nyiberekera ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 150
Sambamba na hayo hadi Sasa mradi umefikia asilimia 65 ya utekelezaji wake ambapo baadhi ya Kazi zinazofanyika ni pamoja na, ujenzi wa nyumba mbili kwa ajili ya mitambo ya maji pamoja na ufungaji wa mabomba ambapo Mradi huu unatarajia kukamilika mwezi Oktoba 2023.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti