Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Nurdini Babu 09/02/2021 amefanya ziara ya Kukagua Miradi ya Maji ndani ya Wilaya ya Serengeti akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Ayub Mwita Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe na Kaimu Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ndugu Wilfred Mwita ambae nae pia aliambatana na Wataalam wake toka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti akiwemo DPLO Martin Mlelema.
Katika ziara hio Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Babu alianzia kukagua Ujenzi wa Chujio la Maji kwenye Bwawa la Manchira pia wamekagua ujenzi wa Mantanki makubwa ya Maji Kijiji cha Kitunguruma ambao umegharimu Tsh Milion 235 mradi ambao utahudumia wananchi zaidi ya 6000.
Pia ziara hio ilifika katika chanzo cha Maji cha Nyamitita Kata ya Ring'wani, na kukagua mradi mwingine kwenye Kijiji cha Nyamitita sehemu ambayo ilimpa fursa Mhandisi wa Maji toka idara ya Maji Muguwasa kuainisha baadhi ya Miradi iliyotengewa fedha.
Gusuhi 235,500,000/=
Maburi 335,500,000/=
Mbalibali 136 Milion.
Monuna 235,500,000/=
Nyambureti 335,000,000/=
Rung'abure 79,900,374.94/=
Makundusi 137,584,685.89/=
Mhandisi pia alielezea changamoto ambazo zinakwamisha wananchi kukosa huduma ya Maji na kutolea mfano wakazi wa Rung'abure ambao wameharibu Generator kwa kuweka Dizel ambayo ilichanganywa na Maji.
Pia alitibitisha juu ya Malipo ya Umeme ambayo tayari wameshalipa Shirika la Tanesco kwa ajili ya kufunga umeme kwenye vituo vyote vyenye miradi ya Maji kiasi cha Tsh 18 milion tayari zimelipwa kukamilisha kazi hio.
Kupitia miradi hio ya Maji Mhandisi wa Maji alithibitisha kuwa Kijiji cha Kebanchancha tayari wametengewa fedh Tsh 80 Milion kwa ajili ya Mradi Mpya wa Maji ambapo pia alitaja vijiji vingine vitakavyo nufaika kuwa ni Kijiji cha Majimoto pamoja na Kijiji cha Nyagansense.
Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Nurdin Babu pamoja na timu walihitimisha ziara yao kwa kutembelea Mradi wa Maji Kijiji cha Makundusi na kukagua Mradi huo ambao umefikia 90% ambapo Mhandisi wa Maji alithibitisha kukabidhi mradi huo kwenye Wiki ya Maji.
Imetolewa
Afisa Habari-Mahusiano
Emmanuel Isyaga Mwita
Halmashauri ya Wilaya Serengeti
tembelea:- www.serengetidc.go.tz
instagram: halmashauriwilaya
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti