Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhandisi Juma Hamsin 16/02/2021 amefanya Kikao na Wafanyabiashara wa Mji wa Mugumu ambao pia ni wamiliki wa vibanda ambavyo vinapatikana ndani ya Halmashauri kikao ambacho pia kimehudhuliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Serengeti Mheshimiwa Ayub Mwita Makuruma pamoja na Wataalam baadhi ambao wanawakilisha Timu ya Ukusanyaji Mapato ya Halmashauri.
Lengo la Kikao hicho na Wafanyabishara hao lilikuwa ni kujadili namna ambavyo wafanyabiashara watalipia Kodi zao za Vibanda kwa Wakati lakini pia wale ambao wana wanadaiwa madni ya pango wanatakiwa kulipa Kodi hizo za Vibanda kulingana na Mikataba yao ilivyoainishwa jambo ambalo litasaidia kuongeza Mapato ya Halmashauri na kuchochea Miradi mikubwa ndani Serengeti.
Katika Kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Juma Hamsini amezungumzia juu ya ujenzi wa Stendi Mpya inayojengwa kwa Mapato ya Ndani huku akiwasihi sana wafanyabishara hao kujenga vibanda maeneo ya Stendi Mpya kwani Vibanda hivo ni vya Gharama nafuu.
Kwa Pamoja viongozi hao wamezungumzia pia suala la Ujenzi wa Uwanja wa Ndege ambao pia utakuwa chanzo cha kikubwa cha mapato Wilayani Serengeti lakini pia utachochea shughuli za Utalii kwani watalii wengi watakuwa wanafika moja kwa moja Serengeti na hivyo huduma za kijamii zitaongezeka na Mapato yatakuwa juu kwa Wafanyabishara watauza vitu vyao kutokna na wageni kuongezeka.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Ayub Mwita Makuruma aliwasihi wafanyabishara hao kuwa masuala ya kulipa kodi ni ya muhimu kwani Kodi hizo ndio zitaongeza Mapato lakini pia hata wao watafanya biashara zao bila kubughuziwa na viongozi wa Wilaya na pia Serengeti itajengwa na wanaserengeti wenyewe hivyo waongeze kasi kwenye masuala ya ulipaji Kodi.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti