Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Ayoub M. Makuruma amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Busawe kwa lengo la kuzungumza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa kata hiyo.
Katika mkutano huo Mhe. Makuruma amewataka wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali kwani imekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ndani ya wilaya ya Serengeti huku akiainisha miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na serikali ndani ya kata ya Busawe.
Aidha, Mhe. Makuruma amewagusa watoto wa kike wanafunzi wa shule ya Sekondari Busawe kwa kutoa msaada wa mipira na taulo za kike na kuaidi kuendelea kuwashika mkono wanafunzi wa shule nyingine ndani ya Wilaya.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti