Mbunge wa chama cha mapinduzi vijana viti maalumu taifa mkoa wa Mara Mhe.Juliana Masaburi amezikumbusha halmshauri kuwa mikopo inayotolewa inahusu wananchi wote na si baadhi ya watu.
Akizungumza na viongozi wa chama na serikali waliofika katika ziara yake ya kutembelea Makundi maalumu yanayofaidika na mikopo ya 10% wilayani Serengeti amewataka viongozi wa halmashauri kutoa mikopi hiyo kwa usawa.
‘’Mikopo itoke kwa wote,wote ni wananchi wa Tanzania wote wanafanyabiashara na wote wanalipa Kodi hii mikopo inatokana na mapato ya Halmashauri’’ alisema Mhe Juliana
Aidha,amezungumzia pia juu ya baadhi ya vijana ambao si waaminifu katika kurejesha mikopo wanayoipata lakini pia kutumia mikopo kwa madhumuni tofauti na yaliyokusidiwa ambayo ni kujikuza kiuchumi na kuweza kujitegemea.Ametoa wito kwa wazazi na walezi kutoa elimu kwa vijana wao juu ya matumizi sahihi ya mikopo hiyo ii kuweza kujitegemea na kuwanufaisha.
Amendelea kuikumbusha wilaya Serengeti kuongeza kiwango cha mkopo iliyotengwa kwa kundi la watu wenye ulemavu lakini pia amewakumbusha watu wenye ulemavu kuwa wanaweza kukopa mikopo hiyo hata kwa mtu binafsi kwa kufata utaratibu.
Sanjari na hayo amezungumzia juu ya njia ya kisasa ya kupokea mikopo yani kwa njia ya mtandao ili kuondoa changamoto mbalimbali za kupokea pesa mkononi.
Mhe Juliana amendelea kuhamasisha juu ya ushiriki katika sensa ya watu na makazi kwa watu wenye ulemavu ili kupata takwimu sahihi ambayo itasaidia serikali katika katika mipango ya Maendeleo na kujua kiasi ambacho kitapelekwa katika eneo husika.Amewataka wazazi kutokuwaficha watu wenye ulemavu.
Akiwa ziarani wilayani Serengeti amechangia Mifuko 50 ya saruji katika ujenzi wa zahanati ya Geitasamo iliyopo nyamerama,ametoa mchango huo wa saruji ili kusaidia zahanati hiyo ambayo itagharimu kiasi chaTsh.Million 24 hadi kukamilika kwake na kuwaomba wadau wa maendeleo mkoani mara kuendelea kumuunga mkono jitihada za Mhe.Rais samia suluhu hassani za kuwaletea Watanzania maendeleo.Lakini pia ametoa mafuta kwa ajili ya Albino ili kukinga ngozi zao zisiweze kudhuriwa.Pia amekabidhi vikundi 5 vya wajasiriamali kiasi cha Tsh 200,000/=
Amewaomba watu wenye ulemavu kutojitenga na kushiriki na kushughuli mbalimbali pamoja na kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Nae katiu wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani serenget Ndg.Ally ally ameimshukuru Mhe.mbunge kwa kufanya ziara katika wilaya ya Serengeti.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti